***********************************
NJOMBE
Jeshi la polisi mkoa wa Njombe linawashikiliwa vijana wawili wanaojulikana kwa majina ya Masoud Mang’ombe na Hamis Ismael kwa tuhuma za kuvunja ofisi ya mahakama ya wilaya ya Njombe na kuiba kopyuta mpakato 3, Mashine moja ya POS na kg 25 za sukari.
Akizungumza na vyombo vya habari kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Njombe Hamisi Issa amesema tukio la kuvunja mahakama na kuiba vitendea kazi na sukari lilitekelezwa mnamo julai 15 na watuhumiwa kukamatwa Septemba 4 mwaka huu.
Katika hatua nyingine Jeshi hilo limesema , siku za hivi karibuni kumeibuka wimbi la wizi wa vipuri vya magari ambapo katika jitihada za kudhibiti uhalifu huo watuhumiwa 6 ambao wanatajwa kuwa kwenye mtandao huo wa wizi wamekamatwa .
Edson Ngimbuchi ni mkazi wa Njombe ambaye pia ni mfanyabiashara ya usafirishaji wa abiria ambaye anasema vitendo vya wizi wa vyombo vya moto na vipuri umekithiri kwa kiasi kikubwa mkoani humo jambo ambalo linawalazimu kulaza vyombo katika maeneo yenye ulinzi.