Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe (kulia)akiteta jambo na Kaimu Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Ziwa, Ahmed Akbarali na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nzega, Suleiman Sekeite katika uzinduzi wa mpango wa kujenga kituo cha huduma kwa wakulima kupitia program ya M-Kulima. Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inakusudia kuanzisha kituo cha mawasiliano cha kidijitali kitakachowawezesha wakulima kuwasiliana na maafisa ugani kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu kilimo.
Kaimu Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Ziwa Ahmed Akbarali akizungumza na wakulima wa mpunga na mahindi wilaya ya Nzega mkoani Tabora katika uzinduzi wa mpango wa kujenga kituo cha huduma kwa wakulima kupitia program ya M-Kulima. Kampuni ya Vodacom Tanzania PLC inakusudia kuanzisha kituo cha mawasiliano cha kidijitali kitakachowawezesha wakulima kuwasiliana na maafisa ugani kuhusu mambo mbalimbali yanayohusu kilimo.