Home Siasa RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAHUTUBIA WAKAZI WA MUSOMA NA KUAHIDI MAKUBWA.

RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AWAHUTUBIA WAKAZI WA MUSOMA NA KUAHIDI MAKUBWA.

0

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma kwa ajili ya kuhutubia wananchi katika mkutano mkubwa wa Kampeni kwa ajili yakuomba kura ili kuchaguliwa  katika uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 28,2020 nchini nzima.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE-MUSOMA)

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoani Mara katika mkutano mkubwa wa Kampeni leo Jumamosi Septemba 5, 2020. Ili kuomba kuchaguliwa katika uchaguzi Mkuu wa Rais ,Wabunge na Madiwani unaotarajiwa kufanyika Jumatano Oktoba 28,2020 nchini nzima.

Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere akizungumza  na wananchi wa mkoa wa Mara na kumuombea Rais kura katika mkutano wa kampeni wa  Mgombea Urais wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama hicho Tawala Rais Dkt John Pombe Magufuli katika uwanja wa Mkendo mjini Musoma mkoa wa Mara 

Mtoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Bw. Makongoro Nyerere akizungumza kwenye mkutano wa kampeni wa Mgombea kupitia chama cha Mapinduzi Rais Dk. John Pombe Magufuli wakati alipomuombea Rais kura kwa wananchi wa Musoma kwenye uwanja wa Mkendo. 

Watoto wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kutoka ni kulia Mkongoro Nyerere na Madaraka Nyerere wakiwa kwenye mkutano huo unliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma.

Mwita Waitara Mgombea Ubunge jimbo la Tarime kupitia Chama cha Mapinduzi CCM akiomba kura za Rais, Wabunge na Madiwani katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma.

Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akifurahia jambo na Mjane wa baba wa Taifa Mama Maria Nyerere katika mkutano wa kampeni wa mgombea kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Dk. John Pombe Magufuli.

Rais Dk. John Pombe Magufuli Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi akifurahia jambo na Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Ndugu Humphrey Polepole wakati Mgombea Ubunge wa Jimbo la Musoma Vijijini Profesa Sospeter Muhongo alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa Musoma katika mkutano wa kampeni uliofanyika uwanja wa Mkendo mjini Musoma.

Msanii Sholo Mwamba mtaalamu wa muziki wa Singeli akitumbuiza katika mkutano wa kampeni wa mgombea Urais Kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma.

Picha Mbalimbali zikionesha Maelfu ya wananchi wakimsikiliza Mgombea Urais kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Dk. John Pombe Magufuli kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye uwanja wa Mkendo mjini Musoma.