Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa India nchini Tanzani. Pembeni yake kulia ni Balozi wa India nchini Mhe. Shri Sanjiv Kohli
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akisaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi wa India nchini Tanzania
………………………………………………………………………..
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Prof. Palamagamba John Kabudi na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Balozi Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge wamesaini kitabu cha maombolezo Ubalozi wa India nchini kufuatia kifo cha Rais mstaafu wa Taifa hilo Shri Pranab Mukherjee kilichotokea tarehe 31 Agosti 2020.
Akizungumza mara baada ya kusaini kitabu cha maombolezo katika ubalozi ubalozi wa India nchini, Jijini Dar es Salaam Prof. Kabudi ametoa pole kwa wananchi wote wa India na kuwasihi kuendelea kuwa watulivu na wastahimilivu wakati huu wa msiba wa kiongozi wao mstaafu.
“Kusaini kitabu cha maombolezo ni ishara ya ushirikiano wetu, umoja wetu na undugu wetu na ndugu zetu wa India. Kifo cha Rais Shri Pranab Mukherjee kinawahusu pia watanzania kwa sababu Tanzania na India zina uhusiano mzuri, imara na wa muda mrefu ulianzishwa na baba wa Taifa Mwl. Julias Nyerere pamoja na Mahatma Gandhi,” amesema Prof. Kabudi
Rais Shri Pranab Mukherjee ni miongoni mwa viongozi wa zamani wa India waliowahi kufanya kazi katika Serikali ya Waziri Mkuu wa Zamani Indira Gandhi aliyewahi kukabidhiwa nyadhifa mbali mbali ikiwemo Waziri katika Sekta tofauti.