Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Donny van de Beek.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Mashetani Wekundu kwa ada ua uhamisho ya Pauni Milioni 40 kutoka kwa vigogo wa Uholanzi, Ajax.
Van de Beek aliyesaini mkataba wa miaka mitano, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi, inaaminika atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 107,000 kwa wiki nje posho.
Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Donny van de Beek PICHA ZAIDI SOMA HAPA
Anakuwa mchezaji mpya wa kwanza kusajiliwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer kuelekea msimu ujao na anatarajiwa kuunda safu nzuri ya kiungo Old Trafford pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.