Afisa Uhusiano VETA,Dora Tesha,akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kwenye bando lao ambapo wameshirika kwenye maonyesho ya Mkutano wa 17 wa siku ya Wahandisi mkutano unaofanyika jijini Dodoma kwa siku mbili.
………………………………………….
Na.Alex Sonna,Dodoma
VETA imetoa wito kwa jamii ya kitanzania na wadau wa sekta ya miundombinu na ujenzi kuhakikisha inawawezesha mafundi stadi nchini ili kuwa nao wengi katika kutekeleza miradi inayotekelezwa hapa nchini.
Wito huo umetolewa leo na Afisa Uhusiano VETA Dora Tesha wakati wa mkutano mkuu wa wahandisi nchini uliofanyika jijini Dodoma.
Aidha Bi. Tesha amesema kuwa ili mhandisi aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufasaha anahitaji mafundi stadi 25 hivyo ni wajibu wetu kuzalisha kwa wingi mafundi stadi katika mamlaka za serikali za mitaa .
“Hivyo sisi kama VETA Kikubwa tunachofanya kwa sasa ni kuhakikisha kuwa mafundi stadi tunao waanzisha wanashiriki katika sekta mbalimbali ambazo wahandisi wanazifanyia kazi ili kupata ujuzi zaidi katika kutekeleza shughuli zao”, amesisitiza Bi. Tesha.
Bi. Tesha ameeleza kuwa jamii na wadau wa miundombinu na ujenzi wanawajibu wa mafunzo ya ufundi stadi yanafika sehemu mbalimbali ili mhandisi aliyepo katika mamlaka za serikali za mitaa asiangaike kutafuta mafundi stadi wa kufanya nao kazi katika maeneo yanayomzunguka.
“Kama tunavyoelewa maendeleo ya viwanda ni sera ya serikali ambayo tunaendelea kutekeleza hadi sasa tumefikia uchumi wa kati lakini jitihada kubwa zinazohitajika naona tunamchango mkubwa wa kufanya ni kuendelea kuhakikisha hawa mafundi stadi wanazalishwa kwa wingi hapa nchini”ameeleza Bi. Tesha.
Bi. Tesha ameongeza kuwa Kwani miradi mingi inatekelezwa hapa nchini mingi inausiana na ujenzi kuboresha mundombinu mbalimbali hivyo tunawajibu mkubwa wa kuzalisha hii nguvu kazi ya mafundi stadi hapa nchini ili kufanya kazi kwani sasa ni wakati wa wazawa kufanya kazi kwa taifa lao.
Tunaona hivi sasa mafundi stadi wanahitajika kwa wingi hivyo mkandarasi mmoja anahitaji kutumia mafundi stadi 25 hivyo ni jukumu la veta kuzalisha mafundi stadi wa kutosha