Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (KWANZA KUSHOTO) akimkaribisha mzazi aliyefika katika banda la chuo hicho ili kupata maelezo ya nanma ya kujiunga na Chuo katika maonesho ya vyuo vikuu Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (KWANZA KULIA) akiteta jambo na Afisa habari wa Chuo hicho Ngaja Mchele wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo.
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (aliyevaa suti)akisalimiana na baadhi ya wawakilishi wa vyuo vilivyohudhuria katika maonesho hayo
Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Waislamu cha Morogoro Prof. Musa Asad (aliyevaa suti)akiwa na Afisa habari wa Chuo hicho wakiteta jambo katika maonesho ya Vyuo Vikuu maeneo ya viwanja vya Mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam
…………………………………………………………………………….
Chuo kikuu cha Waislamu cha Morogoro kinataraji kuongeza kozi mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya jamii katika Nyanja mbalimbali ili kuhakikisha kinatoa wanafunzi wenye weledi katika kukuza uchumi wa Taifa.
Hayo yamebainishwa leo na Makamu Mkuu wa Chuo hicho upande wa Utawala na
fedha Profesa Musa Asad alipotembelea maonesho ya 15 ya Vyuo vikuu nchini yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
fedha Profesa Musa Asad alipotembelea maonesho ya 15 ya Vyuo vikuu nchini yanayoendelea katika viwanja vya mnazi mmoja Jijini Dar es Salaam.
Profesa Asadi amesema Chuo kimeangalia mahitaji ya Taifa katika wakati huu ambao nchi ipo katika uchumi wa kati hivyo inahitaji wataalamu wa fani mbalimbali ambazo zitakuwa sababu ya kukuza uchumi kuelekea viwango vya juu.
Profesa Asad ameongezea kuwa kozi za Afya ni miongoni mwa kozi zitakazoongezwa kutoka zile zilizopo sasa ili kuongeza wataalamu zaidi katika fani hiyo lengo likiwa kumsaidia Mtanzania kuondokana na uhitaji wa kusafiri nje kupata matibabu.
Pamoja na hayo Profesa Asad ameendelea kusema kuwa Chuo hicho kipo katika mkakati wa kuwa kinara katika utunzaji wa mazingira ambapo kuna mpango maalumu wa kugeuza taka zinazozalishwa chuoni hapo kuwa mbolea itakayotuika kukuzia miche itakayooteshwa na chuo hicho.