Mwakilishi wa Vodacom Tanzania PLC, Rehema Kipanga (katikati) akimkabidhi medali ya ushindi wa pili mchezaji wa Namungo, Jamali Issa Dullazi mara baada ya mchezo wa Ngao ya jamii uliofanyika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha jana ambapo mshindi alikuwa timu ya Simba, mchezo huo ulitumika pia kuzindua msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania. Kulia ni mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta.
Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akikabidhi Ngao ya jamii kwa Nahodha wa Simba Sc, John Bocco mara baada ya kutwaa Ngao hiyo ya kuashiria uzinduzi rasmi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania 2020/21. Kushoto ni mkuu wa mkoa wa Arusha Idd Hassan Kimanta.