***************************************
Happy Lazaro, Arusha
Tamasha la muziki wa kizazi kipya lililo washirikisha wasanii ndani ya Mkoa wa Arusha na nje ya Mkoa wa Arusha, limefana na kuwateka vijana wengi wa Mkoa wa Arusha na kuamsha hari ya vijana wengi kuendelea kupenda muziki.
Akizungumza katika Tamasha hilo lililoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arusha na kuwashirikisha wasanii zaidi ya 30 kutoka Arusha huku wasanii wakubwa wakipamba Tamasha hilo wakiwemo Beka Flover,Kala Jeremiah,Dogo Janja,Marioo.
Kennan Kihongosi, amesema kuwa Arusha ilikosa burudani kwa muda mrefu na sasa ni wakati wa kuwapa fursa wasanii kutoka Arusha kuonyesha burudani kwa wana Arusha baada ya Majukumu ya kila siku.
“Kwa kweli tamasha hili la Arusha Festival limekuwa la mfano kwani leo wananchi wangu wameweza kupata burudani ya kutosha na huu ni mwanzo tu,watarajie mambo makubwa chini ya serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dr John Magufuli”Alisema Kennan
Aidha alisema kuwa kufanyika kwa tukio hili linawapa fursa wasanii wa Arusha kuonyesha vipaji vyao na kubadilishana uzoefu na wasanii wakubwa
Kwa upande wake msanii wa Kizazi kipya maarufu kama Dogo Janja amesema kuwa yeye kabla ya kuwa msanii mkubwa alianza kuimba kupitia matamasha kama hayo na amefarijika kuona wana Arusha wamejitokeza kwenye tamasha hilo kuunga Mkono wasanii wa Arusha
Ameongeza kuwa yeye ni msanii kutoka Arusha na ameona baadhi ya wasanii wa Arusha walikuwa hawapatani Lakini kupitia Tamasha hili wamekuwa wamoja na hii ni hatua nzuri,Huku akimpongeza Mkuu wa Wilaya ya Arusha kwa kuanzisha Tamasha hilo ,Arusha Festival.
Kwa upande wao wasanii wa Arusha wamemuahidi ushirikiano Mkuu huyo wa Wilaya pamoja na ofisi yake katika kutoa burudani ndani ya Arusha na viunga vyake.