**************************************
WAZIRI wa ardhi Nyumba maendeleo na makazi WiliamU Lukuvi ameongoza mamia ya waombolezaji mkoani Iringa kumpumzisha aliyewahi kuwa Diwani na makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iringa Onesmo Mtatifiko.
Mtatifikolo amefariki dunia usiku wa kuamkia August 27 katika Hospitali ya Ipamba wilayani Iringa alikokuwa akipatiwa matibabu na kuzikwa August 29/2020.
Marehemu alikuwa mgombea wa udiwani kata ya Idodi tarafa ya Idodi wilayani humo,alikuwa mtoto wa pili kati ya watoto 5 wa Mzee Julius Mtatifikolo, alizaliwa Juni 30/1873 na amefariki August 27/2020 akiwa ameacha mjane na watoto 8 na mjukuu mmoja’’Bwana alitoa na bawana ametwaa jina lake lihimidiwe Amina.
Mazishi hayo yalihudhuriwa na viongozi wa Serikali,Dini,Vyama vya Siasa na wananchi.