Home Siasa DUNIA KUSIMAMA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DODOMA

DUNIA KUSIMAMA UZINDUZI WA KAMPENI ZA CCM DODOMA

0

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maandalizi ya uzinduzi wa kampeni za mgombea Urais wa Chama hicho na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri Kesho.

Jukwaa kuu linavyoonekana.

…………………………………………….

 Katibu wa Itikadi na Uenezi CCM Humphrey Polepole amesema kitu kikubwa kitakachofanyika katika uwanja huo kesho ni kuwaeleza Watanzania sababu za Dk. Magufuli kufanya mambo makubwa ndani ya miaka mitano ya awali ya uongozi wake kabla na kuomba tena ridhaa ya kumalizia kile alichokianza.

“WanaCCM tuna jambo letu. Tumejipanga kuisimamisha dunia. Jambo tulilokuwa nalo si la kubahatisha,” alisema Polepole na kuongeza:

Akizungumza katika maandalizi hayo amesema “Watakuwepo wanasanaa waliopewa vipawa na Mungu kueleza mambo yao kwa ubunifu wa hali ya juu. Tunajua uwanja huu (Jamhuri) hautatosha, hivyo tumeweka maeneo mengi pembeni ya uwanja na kuweka TV kubwa ili waone kinachoendelea.

“Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kutangaza tarehe ya kuanza kampeni ya kuomba dhamana ya kutoa uongozi; tuliamua kutoa siku tatu ili kuseti mitambo yetu. Ratiba itaanza saa moja hadi jioni hadi saa 12 jioni.”

Alibainisha katika saa zote kuanzia asubuhi watakuwa na ubunifu wa kueleza mambo makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano.

Alibainisha kuwa: “Yataelezwa mambo makubwa mara tatu zaidi. Maono ya CCM wakati tunaenda kuomba ridhaa kwa Watanzania.

“Pia matangazo yatarushwa mubashara na vyombo vyote nchini. Kama hutaweza kufika Dodoma ambako sisi tuna jambo letu basi utafuatulia huko huko uliko.
Imekuwa miaka mitano ya mafanikio, miaka mitano ya kumshukuru Mungu itakuw ni miaka mitano ya kufafanua yote mazuri na changamoto tulizokumbana nazo,” alisema Polepole.

“Hakuna chama kilichofikia maandalizi haya. Hata watani zetu leo tumeona mambo yao yalikuwa mpechempeche. Niliwaona namna walivyotepeta.

“Tuna wasaniii 200 ambao wataimba nyimbo 720 tumeziweka pamoja katika kifaa maalum ili baadaye ziweze kutumika. Tumeamua kuwasaidia wasanii wadogo wadogo ili wapate kueleza kile wanachokijua.”

Polepole aliwataja baadhi ya wasanii watakaotumbuiza leo ni pamoja na mwanamuziki mkongwe Hamza kalala, Mrisho Mpoti, Masanja Mkandamizaji na Beka Fkeva.

Wengine ni Mboso, Chid Benz, G Nako, Nandi, Joti. Ali Kiba. Konde Boy na Diamond Platnamz.