Mwandishi wa habari za afya kutoka Full Shangwe Blog akipokea cheti cha ithibati na pongezi mara baada ya kufuzu mafunzo hayo yaliyofanyika kwa siku mbili, leo jijini Dar es Salaam. Kaimu Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya jamii Tanzania (TPHB) Dkt. Julius Massaga akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusiana na namna ya kuripoti habari za afya na kueleza kuwa kupitia jarida hilo la Afya wananchi, wanahabari na watunga sera watapata fursa ya kupata majibu ya maswali yao kupitia tafiti mbalimbali zilizochapishwa katika jarida hilo, leo jijini Dar es Salaam.Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Ukuzaji Tafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mary Mayige akizungumza na waandishi wa habari za afya leo jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo ya maalumu ya kuwajengea uwezo wanahabari katika kuripoti habari za afya.
Viongozi mbalimbali kutokaTanzania Public Health Bulletin (TPHB), Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) wakiwa katika picha ya pamoja na waandishi wa habari za afya walioshiriki mafunzo maalamu ya kuwajengea uwezo leo jijini Dar es Salaam.
……………………………………………..
NA NOEL RUKANUGA
Waandishi wa habari za Afya nchini wametakiwa kuripoti taarifa kwa kuzingatia maadili ya taaluma yao kwa kufuata sheria jambo ambalo litasaidia kutoa majibu kuhusu masuala mbalimbali katika sekta ya afya pamoja na kuepuka habari ambayo inaweza kujenga hofu katika jamii.
Wito huo umetolewa leo jiji Dar es Salaam na Kaimu Mhariri mkuu wa Jarida la Afya ya Jamii Tanzania (TPHB) Dkt.Julius Massaga wakati akitoa somo kwa waandishi wa habari kuhusu namna bora ya kuripoti taarifa za afya.
Dkt. Massaga amesema kuwa lengo la kutoa semina kwa waandishi wa habari ni kuwajengea uwezo ambao utawasaidia kuripoti taarifa za afya kutoka vyanzo vya habari vilivyokuwa sahihi.
” Tumetoa semina kwa wanahabari kwa siku mbili ili kuwasaidia waripoti habari za kweli na kuepuka kutoa taarifa ambazo zinaweza kuleta hofu kwa wananchi” amesema Dkt. Massaga.
Kaimu Mkurugenzi wa Uratibu na Ukuzaji Tafiti kutoka Taasisi ya utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) Dkt. Mary Mayige, amesema kuwa mafunzo hayo maalumu kwa wanahabari yanakwenda kuwajengea uwezo katika kuripoti habari za afya.
Dkt. Mayinge amesema kuwa wapo tayari wakati wowote kutoa taarifa na ufafanuzi kwa waandishi wa habari ili kuhakikisha wapata taarifa sahihi.
Hata hvyo ameawata waandishi wa habari kuyafanyia kazi kwa vitendo yale ambayo wamefundisha ili kuleta matokeo chanya katika jamii.
Semina hiyo imeandaliwa na Tanzania Public Health Bulletin (TPHB) kwa kushirikiana na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa kutoa mafunzo maalumu kuhusiana na namna bora ya kuripoti habari za afya ambapo kupitia mradi wa Takwimu na Sera za afya kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo, Wizara ya afya, Taasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) na ofisi ya mganga mkuu wa Serikali.
Uwepo wa jarida la Afya nchini wamerahisisha namna ya kupata taarifa muhimu za afya kupitia jarida hilo ambalo limesheheni taarifa na matokeo ya tafiti mbalimbali za kisayansi