Home Mchanganyiko MLOGANZILA YAKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI

MLOGANZILA YAKABIDHIWA CHETI CHA SHUKRANI

0

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga & Mloganzila Prof .Lawrence Museru (katikati), pamoja na Kaimu Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Muhimbili – Mloganzila (kushoto) Dkt. Julieth Magandi wakipokea cheti cha shukrani kutoka kwa mwakilishi wa Familia ya Wanyumbani Bw. Fakihi Rashid Bakiri.

Fakihi Rashidi Bakiri (wakwanza ) kushoto akizungumza kwaniaba ya Familia ya Wanyumbani walipofika Hospitali ya Mloganzila kwa lengo la kushukuru kwa huduma aliyopatiwa ndugu yao na afya yake kuimarika.

Prof .Lawrence Museru akizungumza na ndugu wa Familia ya Wanyumbani pamoja na baadhi ya watalamu ambao walikuwa wakimuhudumia mgonjwahuyo.

Museru akiwa katika picha ya pamoja na wataalamu wa MNH-Mloganzila pamoja na wawakilishi kutoka Familia ya Wanyumbani.

………………………………………………………..

Familia ya Wanyumbani ya Jijini Dar es salaam wamekabidhi cheti cha shukrani kwa Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila baada ya ndugu yao aliyepooza kupatiwa matibabu na afya yake kuimarika.

Akizungumza kwaniaba ya familia Bw.Fakihi Rashidi Bakiri amesema ndugu yao alipatarufaa ya kuja MNH-Mloganzila tarehe 9 Agosti 2020 hali yake ikiwambaya, kwani alikuahaoni wala hasikii chochote hivyo hawakutegemea kama afya yake ingeimarika.

 “Tunawashukuru Wauguzi, Madaktari na watoahuduma wote kwa ujumla kwa kumuhudumia ndugu yetu kwani hatukutegemea kama angeweza kuona na kuongea tena baada ya kupooza kwa muda wa takribani mwezi mmoja”amesema Bw. Bakiri.

Bw. Bakiri ametumia fursa hiyo kuitaka jamii kuondokana na dhana potofu na kupuuza maneno yanayosemwa na baadhi ya watu kwamba mgonjwa akipelekwa Mloganzila haponi, habari hizo sizakweli na badala yake jamii inapaswa kuweka imani kwa Hospitali ya Mloganzila kwani wanatoahuduma bora na wanajituma kwamoyo.

“Tulipatamshtuko baada ya kuambiwa kwamba mgonjwa wetu amepewa rufaa ya kwenda Mloganzila ,tukajua hatapona tena ila tunamshukuru Mungu amehudumiwa vizuri na ndio maana tumekuja kuwakabidhi cheti hiki kama ishara ya shukrani kwa kuhuduma zenu kwa wagonjwa”.  Amefafanua Bw. Bakiri.

Kwaupande wake Mkurugenzi Mtendandaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Upanga & Mloganzila Prof. Lawrence Museru ameishukuru familia ya Wanyumbuni kwa kuthamini mchango wa wataalamu wa afya ambao wamekuamstari wa mbele kuhakikisha wanatoa huduma kwa wagonjwa wote wanaofika hospitalini hivyo shukrani hizo ni chachu ya kuongeza juhudi katika utoaji huduma bora za afya.

Prof.Museru amesisitiza kwamba Hospitali ya Mloganzila itaendelea kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote na kuhakikisha wanapata matibabu stahiki na kwa wakati .