Home Mchanganyiko DKT. KAZI ATOA WITO KWA WADAU KUWEKEZA KATIKA MKOA WA RUVUMA

DKT. KAZI ATOA WITO KWA WADAU KUWEKEZA KATIKA MKOA WA RUVUMA

0

…………………………………………………..

Na. Mwandishi wetu, Ruvuma

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania-TIC Dkt. Maduhu Kazi amesema Mkoa wa Ruvuma unazo fursa nyingi za Uwekezaji na kuwakaribisha wadau kuwekeza katika sekta mbalimbali ndani ya mkoa huo.

Amezitaja fursa hizo kuwa ni pamoja na Uwekezaji kwa upande wa makaa ya mawe, viwanda vya mbolea, sekta ya utalii kwa ujenzi wa hoteli za kisasa pamoja na kilimo cha mazao mbalimbali ambayo yamekuwa na tija ya kiuchumi.

Dkt.Kazi yupo ziarani Ruvuma akikagua maendeleo ya shughuli za Uwekezaji.

Amesema jukumu la TIC ni pamoja na kusimamia, kuhamasisha na kuvutia Uwekezaji na hivyo wawekezaji ni wakati wao sasa kuwekeza Ruvuma.

“Ruvuma kuna fursa nyingi, wawekezaji tunawaomba mje kuwekeza huku, kuna fursa katika sekta ya uchimbaji wa makaa ya mawe, kilimo, viwanda vya mbele, ujenzi wa hoteli za kisasa na nyingine nyingi, sisi TIC tutawasimamia vizuri” alisema Dkt.Kazi.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Ruvuma Stephen Ndaki alisema Mkoa huo umejiandaa kupokea wawekezaji na kiwahudumia.

“Ruvuma tupo vizuri, tumejiandaa na tumeandaa mazingira mazuri kwa wawekezaji wetu wote watakaokuja kuwekeza” alisema Bw.Ndaki.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Songea Pollet Kamando alisema kuna mazingira mazuri ya Uwekezaji katika  Wilaya yake.

Katika ziara hiyo Dkt. Maduhu alitembelea pia shamba la kisasa la Ndolela kujionea hali ya Uwekezaji katika Shamba hilo ambalo linazalisha mazao mbalimbali  mchanganyiko na mifugo  kwa ujumla lina ukubwa wa ekari elf 5.