****************************
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
LINACHUNGUZA KIFO CHA MTU MMOJA
MWANAFUNZI NA WATU WENGINE 18
WALIOATHIRIKA KWA KILE KINACHODAIWA
KULA CHAKULA CHENYE SUMU.
TEREHE 24.08.2020 MAJIRA YA 16:00HRS HUKO KITUO
CHA AFYA MWANGIKA, KATA YA BANGWE, WILAYA
YA SENGEREMA, MKOA WA MWANZA. MBONI
MAHANO, MKEREWE, MIAKA 13, MWANAFUNZI,
DARASA LA SABA SHULE YA MSINGI MWANGIKA.
ALIFARIKI DUNIA AKIWA ANAPATIWA MATIBABU
KATIKA KITUO CHA AFYA MWANGIKA BAADA YA
KUDAIWA KULA CHAKULA KINACHODAIWA KUWA
NA SUMU ALIPOKUWA KWENYE SHEREHE. MWILI WA
MAREHEMU UMEHIFADHIWA KITUO CHA AFYA
MWANGIKA KWA UCHUNGUZI WA DAKTARI.
UCHUNGUZI WA AWALI AMEBAINI KUWA TAREHE
22.08.2020 KULIFANYIKA HARUSI NYUMBANI KWA
DORICA OMAJIGO AMBAPO WATU WALIKULA
CHAKULA NA KINGINE KILIBAKI. TEREHE 23.08.2020
WANAWAKE NA WATOTO WAO WALIRUDI
KUSAFISHA VYOMBO NDIPO WAKALA TENA
CHAKULA KILICHOBAKI, BAADA YA MASAA
KADHAA WALIANZA KUUMWA NA KUKIMBIZWA
KATIKA KITUO CHA AFYA MWANGIKA AMBAPO
WATU WAZIMA 04 NA WATOTO 14 WAMELAZWA
KWA MATIBABU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAFATILIA
KWA KARIBU TUKIO HILO, NA HALITASITA
KUCHUKUA HATUA KALI ZA KISHERIA KWA YEYOTE
ATAKAYEBAINIKA KUHUSIKA NA KITENDO HICHO
BAADA YA UCHUNGUZI.