Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kushoto akisalimia kwa furaha na Mwenyekiti mpya wa baraza jipya la ardhi na nyumba la Wilayani Mafia Rehema Mwakibuja nje ya jengo la Ofisi ya Mkuu wa Wilaya mara tu baada ya kumalizika kwa halfa fupi ya kuapishwa kwa wajumbe hapo ambapo kulihudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali.
Baadhi ya viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Mafia pamoja na Mkoa wa Pwani wakiwa wanashuhudia zoezi la Mkuu wa Mkoa wa Pwani kuwaapisha kwa wajumbe wa baraza hilo la ardhi hawap pichani pamoja na Mwenyekiti wao.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere akizungumza jambo na viongozi mbali mbali wa Wilayani Mafia pamoja na wananchi wakati wa ziara ya kikazi ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani yenye lengo la kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi.
Mwenyekiti wa baraza jipya la ardhi na nyumba la Wilayani Mafia Rehema Mwakibuja akiwa amesimama kwa ajili ya kusubilia kuapishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani kwa ajili ya kuanza kutekeleza majukumu yake ya kuwatumikia wananchi wa Wilaya ya Mafia katika kuwaikiliza na ktatua changamoto zao.
Mwonekano wa picha ya Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa na viongozi mbali mbali wa serikali pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Mafia ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
Mwenyekiti wa baraza jipya la ardhi na nyumba la Wilayani Mafia Rehema Mwakibuja kulia akipena mkono huku akicheza kwa furaha na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa baraza jipya la ardhi la Wilaya pamoja na kuapishwa kwa wajumbe.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
…………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, MAFIA
SERIKALI Mkoa wa Pwani katika kukabiliana na wimbi la kuwepo kwa migogoro ya mipaka ya ardhi ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara imezindua rasmi baraza la ardhi na nyumba la Wilaya ya Mafia kwa lengo la kuweza kusikiliza na kusuluhisha kesi mbali mbali ambazo zimekuwa zikijitokeza ili ziweze kutafutiwa ufumbuzi kwa kuzingatia sheria na taratibu za nchi.
Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa uzinduzi rasmi wa baraza hilo la ardhi uliokwenda sambamba na kuwaapisha wajumbe watatu akiwemo na Mwenyekiti wao na kukemea vitendo vya kuwaonea wananchi na badala yake wahakikishe kwamba wanatenda haki na kusikiliza kesi kwa wakati na kuachana na kufanya kazi kwa mazoea.
“Sisi kama serikali ya Mkoa wa Pwani tuaamua kumwandikia mapendekezo yetu maalummu Waziri wa ardhi nyumba maendeleo na makazi Wiliam Lukuvi na kitu cha kufurahisha aliyakubali na pia alitukubalia kuunda baraza hili la ardhi la Wilaya ya Mafia ambalo nina imani litaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa wananchi katika kutatuliwa kero na changamoto katika suala zima la ardhi,”alisema Ndikilo.
Ndikilo alibainisha kwamba kuanzishwa kwa baraza hilo la ardhi katika Wilaya ya Mafia kutawaondolea kwa kiasi kikubwa adha wananchi ambayo waliyokuwa wanaipata kwa kipindi cha muda mrefu cha kusafiri umbari mrefu kwenda katika Wilaya nyingine za Mkuranga kwa ajili ya kupeleka malalamiko na kesi zao ili ziweze kusikilizwa.
Aliongeza kuwa katika Mkoa wa Pwani kumekuwepo na migogoro mingi ya ardhi ikiwemo Wilaya ya Mafia hivyo baraza hiyo litasaidia katika kuzisikiliza kero za wananchi ambazo zilikuwa zikiwakabili kwa kipindi kirefu bila ya kutafutiwa ufumbuzi na kwamba amewataka wajumbe hao kuhakikisha wanafanya kazi kwa weledi.
“Hapa nimefanya zoezi la kuwaapisha wajumbe watatu wa pamoja na mwenyekiti wao mpya wa baraza hili la ardhi kwa hivyo sasa kitu kikubwa mnatakiwa kuchapa kazi kweli kweli kwa ajili ya kuwatumikia wananchi wa Mafia isije sasa kuoana tena wananchi hawa wanaanza kuzungushwa kwa miaka miwili hadi mitatu kesi zao bado zinasikilizwa tu katika hili naomba sana muweke mipango mizuri ya kuziwaisha kesi zao,”alisema Ndikilo.
Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Pwani Dk. Delphine Magere aliwatakaviongozi walioapishwa katika baraza hilo kutimiza majukumu yao ipasavyo katika kuwatetea wananchi wa Wilaya ya Mafia na kwamba serikali ya Mkoa wa Pwani itaendelea kuwapa ushirikiano wa kutosha katika kutatua changamoto mbali mbali lengo ikiwa ni kuleta chachu ya maendeleo kwa wananchi wote.
“Hii ni fursa sasa kwa wananachi wa Wilaya ya Mafia amabo hapo awali walikjuwa wanakabiliwa na tatizo la kusikilizwa kesi zao lakini kwa sasa nadhani hii itakuwa ni njia moja wapo ya kuwasaidia wananchi ambao walikuwa wanapatwa na matatizo ya ardhi lakini kutokana na kuwepo kwa uundwaji wa baraza hili itakuwa ni msaada mkubwa katika jambo hili,”alisema Magere.
Naye Mwenyekiti wa baraza jipya la ardhi na nyumba la Wilayani Mafia Rehema Mwakibuja amesema kwamba atahakikisha anatekeleza maagizo yote ambayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani ikiwemo kusimamia na kutoa haki sawa bila ya kuwepo kwa upendeleo n aubaguzi wowote kwa kuzingatia sheria na taratibu zilizowekwa za nchi.
Nao baadhi ya wajumbe ambao wameteuliwa kuunda baraza hilo wamesema kwamba kutokana na kuwepo kwa migogoro mingi ya ardhi katika Wilaya ya Mafia watajitahidi kadiri ya uwezo wao katika kusuluhisha na kufanya maamuzi yaliyo sahihi katika kesi mbali mbali ambazo zitawafikia mezani kwao.
Kuundwa kwa mabaraza mapya ya ardhi na nyumba katika Wilaya ya Mafia iliyopo Mkoa wa Pwani kutaweza kusaidia kupunguza changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zinawakabili wananchi hao ambao hapo awali walikuwa wanasafiri umbari mrefu wa kwenda hadi Wilaya nyingine kwenda kusikiliza kesi zao.