Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akirudisha Fomu ya Kugombea nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika tarehe 28 Oktoba, 2020 kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakipokea Seti moja ya Fomu ya Uteuzi 8A, Fomu namba 10 pamoja na Picha za Wagombea kutoka kwa Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage pamoja na Mkurugenzi wa NEC Dkt. Wilson Charles wakihakiki Fomu za Mgombea Urais kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi CCM Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage (aliyesimama) akitangaza kumteua Mgombea wa kiti cha
(Urais) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kurejesha fomu za uteuzi kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.
(Urais) Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Mgombea Mwenza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan baada ya kurejesha fomu za uteuzi kwenye ofisi za Tume zilizopo Njedengwa jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akitoa Fomu zake na kuzihakiki mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakati akisaini Fomu katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Fomu zake kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi kutoka NEC Dkt. Wilson Charles kwa ajili ya uhakiki katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakimsikiliza Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC Jaji Mstaafu Semistocles Kaijage katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC Njedengwa jijini Dodoma .
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Wafanyakazi wa NEC mara baada ya kurejesha Fomu na kuteuliwa kuwa Mgombea kupitia Tiketi ya CCM Njedengwa jijini Dodoma.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgombea Mwenza Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan wakiwasili katika Ofisi za Makao Makuu ya NEC jijini Dodoma kwa ajili ya kurejesha Fomu.
PICHA NA IKULU
………………………………………………..
Uteuzi huo umefanyika leo jijini Dodoma katika Ofisi za Tume ya Taifa ya Uchaguzi mara baada ya Dkt.Magufuli na Mgombea Mwenza waliporudisha fomu za uteuzi kutoka NEC na kuonekana kuwa wamekidhi sifa za kugombea kupitia CCM.
Katika safari yake ya kutafuta wadhamini, Dkt. Magufuli amepata wadhamini kutoka Mikoa 15 kutoka Tanzania bara pamoja na Visiwani huku pia akikabidhi stakabadhi ya malipo ya kiasi cha Shilingi Milioni 1 na wote wameapa kwa Jaji wa Mahakama Kuu.
Zoezi la urejeshaji wa fomu za uteuzi kwa nafasi ya Urais, Ubunge na Udiwani kutoka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), litahitimishwa leo majira ya saa 10:00 jioni