Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba leo,Akiwapongeza Walimu wa Sekondari ya Mbamba bay kwa kufaulisha kidato cha sit kwa asilimia 100.amewataka wafaulishe kidato cha nne kwa asilimia 100 tena kwa uwezo wanao. Picha na Ofisi ya Ded Nyasa
………………………………………………………………..
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa Bi Isabela Chilumba leo amefanya ziara ya kikazi katika Shule ya Sekondari ya Limbo, iliyopo Kata ya Kilosa, na Shule ya Sekondari ya Mbamba bay Iliyopo, Kata ya Mbamba bay wilayani hapa.
Ziara hiyo ina lengo la kutatua changamoto katika shule zote za Sekondari Wilayani hapa, ili kuongeza Ufaulu wa wanafunzi wa Kidato Cha Nne na kuwapongeza Walimu wa Sekondari ya Mbamba bay, kwa kufaulisha vizuri wanafunzi wa Kidato cha Sita.
Bi Chilumba amefafanua kuwa anachohitaji ni kuona wanafunzi wa Kidato cha nne wanafaulu kama wale wa kidato cha sita kwa kuwa walimu ni hao hao.
Akiongea na Walimu wa Limbo Sekondari, amewataka kufanya kazi kwa kufuata maadili ya kazi , na kuwafundisha wanafunzi kwa Upendo na kuwafuatilia, Shuleni na Nyumbani, na kuwapa mazoezi ya mara kwa mara, ili waweze kujisomea na kujifunza wawapo shuleni na Nyumbani ili kuongeza ari ya kujifunza.
Ametoa wito kwa Walimu wa Shule hiyo kufundisha kwa bidii na kuacha visingizio mbalimbali, kwa kuwa wao kama wataalamu wa elimu wamepelekwa mashuleni ili
kuwafundisha wanafunzi , wazazi, na wanajamii kutatua changamoto ili kuleta mabadiliko katika maeneo yao ya Kazi.
Aidha amewaagiza wakaguzi wa Elimu Wilayani Nyasa kupeleka nakala ya Taarifa ya ukaguzi na kusema kuwa, hatawavumilia walimu wazembe, ambao hawatafaulisha
kwa kuwa malengo ya kila mwalimu ni kuhakikisha wanafunzi wake wanafaulu masomo anayofundisha na kamwe hatamvumilia mwalimu mzembe
“Nawaagiza walimu wakuu na wakaguzi wa elimu wilayani hapa kwamba, hamtakiwi
kuwavumilia walimu wazembe ambao hawafaulishi, kazi yao ni kutoa visingizio,
hatuwezi kufikia hapo tunatakiwa kubadilika, na kuhakikisha wanafunzi wanafaulu kwa
kila masomo yenu mnayofundisha. Lakini pia tunatakiwa kuwa na malengo ya kuhakikisha kuwa wanafunzi wanafaulu kwa hali yoyote ile”.Alisema Chilumba.
Katika shule ya Sekondari ya Mbamba Bay Amewapongeza walimu wa Shule hiyo kwa
kufaulisha wanafuzi wote wa Kidato cha sita na kuwataka matokeo kama hayo
yapatikane kidato cha nne, na mbinu walizotumia kufundisha Kidato cha sita wazitumie
kufaulisha Kidato cha nne.
Aidha amewashuru na kuwapongeza wananchi wa Wilaya ya Nyasa, kupitia ukurasa
wa kijamii wa Facebook wa Nyasa kwetu Forum kwa kufuatilia habari za Nyasa na
kuchangia kwa umakini mada zinazohusu uboreshaji wa Elimu, miundombinu,na
masuala mengine ya Kijamii Kwa Wilaya ya Nyasa.
Awali walimu hao walizitaja changamoto wanazokutana nazo ni pamoja na Kutopata
ushirikiano na wazazi, kwa kuwahamasisha wanafunzi kusoma ,kutochangia chakula
na kuwafanya wanafunzi kusoma na njaa, kutembea umbali mrefu na kufika shule
wakiwa wamechoka na kutomudu masomo.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa bw. Jimson Mhagama
aliwataka walimu kuhakikisha wanafundisha na kuhakikisha wanafunzi wanafaulu ili
kufikia malengo ya Wilaya ya kufaulisha wanafunzi wote wa Kidato cha Nne, kwa kutoa
Elimu kwa wazazi na walezi kwa kuwa wazazi wengine hawana ufahamu juu ya kutoa
ushirikiano kwa walimu ili kuinua kiwango cha Elimu Wilayani Nyasa.
Mkuu wa Wilaya ya Nyasa katika ziara hiyo aliambatana na Kamati ya Ulizi na Usalama
Wilaya ya Nyasa.Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa na Wakuu wa Idara za Elimu
Sekondari,Elimu Msingi, Tume ya Utumishi wa Walimu, na Mkuu wa Idara ya Utawala
na Raslimali Watu Bw.Liston Moyo.
Matokeo ya Kidato cha sita katika Wilaya ya nyasa 2020 wamefaulu kwa asilimia 100%
kwa shule zote Mbambabay Sec. Na St. Pauls' Sec.
Mbambabay: Div I->53, II->88, III->13, ->: 0, O->0.
ST. PAULS: I->13, II->45, III->19, IV->0, O->0. Shule zote ufaulu wa 100%