Home Michezo YANGA YAMTAMBULISHA SENZO KUWA MSHAURI WA KLABU

YANGA YAMTAMBULISHA SENZO KUWA MSHAURI WA KLABU

0

******************************

Klabu ya Yanga leo imemtambulisha senzo Mazingisa kuwa Mshauri wao baada ya kuondoka kutoka mwa mahasimu wao Simba na kujiunga na klabu hiyo hivi karibuni.

Akizungumza na Vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam Mwenyikiti wa Klabu ya Yanga Dkt.Mshindo Msolla amesema wameamua kumtambulisha Snzo hii leo pia wanaendelea kujipanga kwaajili ya msimu ujao na matarajio yao ni kufanya vizuri.

“Yanga SC tunamtambulisha rasmi Senzo kuwa mshauri wetu, atakuwa hapa kalbuni pia na GSM kwenye mazungumzo ya mabadiliko ya mfumo mpya wa uendeshaji wa klabu yetu kushirikiana na La Liga na Sevilla, kuanzia leo mnaweza kumhoji kuhusu Yanga.” -Dkt. Mshindo Msolla, M/Kiti wa Yanga.

Kwa Upande wake Senzo amesema atakuwa mshauri na kuiunganisha kati ya La liga, Sevilla na yanga na kutoa ushirikiano na uongozi wa klabu.

“Nitakuwa mshauri na kiunganishi kati ya La Liga & Sevilla pamoja na Yanga SC, nitatoa ushirikiano wangu wote kwa kushirikiana na viongozi wa Klabu pamoja na GSM kuleta mafanikio ndani ya Klabu, sasa najisikia mwanafamilia wa Yanga SC.” – Senzo, Mshauri wa Yanga SC.

Aidha Senzo amesema kuwa si rahisi kujiunga na yanga kwasababu ni moja ya klabu kubwa barani Afrika hivyo basi kwak ni bahati kubwa kujiunga na klabu hiyo.

“Si kazi rahisi kujiunga na Yanga SC kwa sababu ni moja ya klabu kongwe, kubwa na yenye historia nzuri Barani Afrika. Kwangu ni bahati, nitafanya kazi ya kuishauri klabu na kuhakikisha tunaingia kwenye mfumo mpya, wa kisasa kuiongoza klabu ili kuwa tayari kushindana.” – Senzo.