Home Mchanganyiko TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA

0

******************************

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAMSHIKILIA
MSAIDIZI WA KAZI ZA NDANI KWA TUHUMA ZA KOSA LA
KUMUUA MTOTO MDOGO WA MWAJIRI WAKE.

TAREHE 23.08.2020 MAJIRA YA 10:30HRS HUKO KATA YA
ILOGANZALA, WILAYA YA ILEMELA, MKOA WA MWANZA,
MTOTO MDOGO MWENYE UMRI WA MIEZI 11 ANAYEITWA
KELVIN KASTUS, MUHA, MKAZI WA ILOGANZALA,

ALIUAWA KWA KUZIBWA PUMZI KWA KUTUMIA SHUKA NA
MSAIDIZI WA KAZI ZA NDANI AITWAYE ASHURA SUKA,
MIAKA 15, MSUKUMA, MKAZI WA NYAMANORO NA
KUSABABISHA KIFO CHAKE.

CHANZO CHA MAUAJI HAYO KINACHUNGUZWA KWA KINA
NA UPELELEZI UTAKAMILISHWA HARAKA KADRI
IWEZEKANAVYO, MTUHUMIWA ATAFIKISHWA
MAHAKAMANI. MWILI WA MAREHEMU UMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA YA SEKOU TOURE KWA
UCHUNGUZI WA DAKTARI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWATAKA WAZAZI
NA WALEZI WENYE WATOTO WADOGO KUJENGA
UTAMADUNI WA KUAJIRI WATU WANAO WAFAHAMU
TABIA, MIENENDO NA MALEZI YA WAHUSIKA KWANI NI
HATARI KUMWACHIA MTU USIYE MFAHAMU VIZURI
AKUFANYIE KAZI YA MALEZI YA MTOTO MDOGO.