Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Bw. Patience Ntwina akitoa maelezo kwa watalaam wa kikao kazi kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali wanaofanya mapitio ya kanuni ya adhabu sura ya 16 mjini Morogoro chenye lengo la kuondoa maneno, maudhui na adhabu zilizopitwa na wakati.
Wataalam wakiendelea na majadiliano.
***********************************
Mkurugenzi wa Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki wa Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina afungua kikao kazi kuhusu mapitio ya sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16.
Kikao kazi hicho cha siku 12 kinafanyika katika ukumbi wa TFS-Mbegu mjini Morogoro kinajumuisha wataalam kutoka Wizara, Idara na Taasisi za Serikali.
Mkurugenzi Ntwina akizungumza na wataalam hao amesema “Wizara imepanga kufanya zoezi la mapitio ya sheria hii ili kuondoa maneno, maudhui na adhabu zisizoendana na wakati tuliono sasa”.
Katika kikao kazi hicho wataalam hao wanajadii namna ya kuondoa maneno, maudhui na adhabu zilizopitwa na wakati na kutoa mapendekezo juu ya nini kifanyike ili kuhuisha adhabu hizo ili ziendane na wakati kwani kwa sasa zinashindwa kushughulikia matukio ya uhalifu
yanayotokea kwenye jamii.
Aidha, wataalam hao pia watapitia vifungu vya sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai na uhujumu uchumi na kuandaa mapendekezo yatakayotumika kuweka utaratibu na mwenendo mzuri wa kushughulikia kesi katika mahakama kuu ili kupunguza mlundikano wa mahabusu
katika magereza.
Sheria ya kanuni ya adhabu sura ya 16 ilitungwa wakati wa utawala wa kikoloni na imekuwa ikifanyiwa marekebisho mbalimbali ya vifungu yaliyogusa kushughulikia mahitaji yaliyojitokeza katika jamiii.