Mhandisi wa Ujenzi, Shirila la Viwango Tanzania(TBS), Eng.Innocent Johnbosco akizungumza na wanahabari katika ofisi za Shirika hilo Jijini Dar es Salaam.
*********************************
NA MWANDISHI WETU
Wananchi wameshauriwa kutumia Marumaru (Tiles) kwa matumizi maalumu katika kujengea ili kuepukana na madhara makubwa kujitokeza.
Ameyasema hayo leo Mhandisi wa Ujenzi, Shirila la Viwango Tanzania(TBS), Eng.Innocent Johnbosco katika ofisi za shirika hilo, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na Wanahabari, Eng.Innocent amesema madhara ya kutumia tiles ambazo si sahihi au mahala si sahihi inaweza kuleta madhara kama kuteleza na kusababisha madhara makubwa kimwili.
“Wengine wanaweza wakawa wanazalisha wanatumia madini ambayo yameshakatazwa na bahati nzuri hatuna hizo kesi hapa kwetu lakini kuna wengine wanaweza kuchanganya baadhi ya madini ambayo yanamadhara kwa binadamu”. Amesema Eng.Innocent.
Amesema kwa mujibu wa Viwango kunakiwango cha Marumaru (Tiles) namba 954 ambacho kinazungumzia ubora na namna gani unaweza kufikia ubora wa tiles za sakafuni na ukutani.
Aidha Eng.Innocent amesema kuwa kupitia Viwango namba 954 cha mwaka 2018, viwango vinagawanyika kutegemea na namna ya uzalishaji lakini na namna marumaru hizo kunyonya maji lakini mbali zaidi kuna uwezo wa kuhimili kiasi gani cha michubuko.
“Katika kiwango hicho namba 954 kimefafanua namna gani ya kufikia ubora hasa kwa wasalishaji wetu wa ndani ili waweze kuzalisha vigae ambavyo vinakidhi matakwa ya soko lakini inakidhi malengo yaliyokusudiwa kwaajili ya matumizi”. Amesema Eng.Innocent.
Pamoja na hayo Eng.Innocent amesema ili kuweza kujiridhisha na ubora wa marumaru, kwenye kifungashio cha marumaru kwa wale wazalishaji wa ndani wanatakiwa kufuata matakwa ya kiwango hasa kutaja kiwango ambacho kimetumika katika uzalishaji wa marumaru pia waandike ni aina gani ya marumaru iliyopo humo ndani kwa maana kuna aina nyingi za tiles ambazo zinatumika katika matumizi mbalimbali.