Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadhibiti wa ubora wa elimu wa Mikoa chenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kuwatambua wabunifu katika maeneo yao kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadhibiti wa ubora wa elimu wa Mikoa chenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kuwatambua wabunifu katika maeneo yao kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula akitoa taarifa wakati wa ufunguzi wa kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadhibiti wa ubora wa elimu wa Mikoa chenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kuwatambua wabunifu katika maeneo yao kilichofanyika leo jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe akiwa katika picha mbalimbali na washiriki mara baada ya kufungua kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadhibiti wa ubora wa elimu wa Mikoa chenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kuwatambua wabunifu katika maeneo yao kilichofanyika leo jijini Dodoma.
………………………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Serikali kupitia Wizara ya Elimu imesema kuwaa itaendelea kuboresha bunifu na Teknolojia mbalimbali hapa nchini kwa Sasa imeboresha uratibu wa upatikanaji wa bunifu hizo ili ziendelezwa kwa manufaa ya Taifa.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. James Mdoe wakati wa kufungua kikao kazi na Maafisa Maendeleo ya Jamii na wadhibiti wa ubora wa elimu wa Mikoa chenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kuwatambua wabunifu katika maeneo yao.
Prof.Mdoe amesema kuwa kwa Sasa Wizara inayaboresha mashindano ya kuwapata wabunifu wa teknolojia sambamba na kuboresha uratibu wa zoezi hilo.
” Ubunifu wa Teknolojia ni muhimu Sana kwa kwa taifa na sisi kama Wizara tunaboresha hasa uratibu wa zoezi la kuwavumbua wabunifu wa teknolojia na kuwaendeleza”
Ameongeza kuwa ” kwa mwaka 2020 – 2021 tumetenga milioni mia nane sabini na nne (874) ili kuzitambua na kuziendeleza bunifu katika makundi mbalimbali” amesema Prof. Mdoe.
Hata hivyo amesema kuwa tangu kuanza kwa mashindano hayo Wizara imeweza kuibua bunifu 1066 na bunifu 130 zimeendelezwa na Kati ya hizo zipo katika hatua ya mwisho katika kuingizwa sokoni ili ziweze kuchangia katika uchumi wa taifa.
Prof.Mdoe amesema kuwa kwa kipindi ambacho wameanza kuibua Teknolojia hizo kumekuwa na changamoto mbalimbali ikiwamo changamoto ya uelewa mdogo kwa jamii hasa maeneo vijijini.
” Ndio maana tumewaita hapa maafisa Maendeleo ya jamii na Maafisa udhibiti ubora ili mtusaidie kufikia elimu hiyo kwa sababu ninyi mnafanya kazi na makundi yote na Maafisa udhibiti ubora mnapopita katika shule muangalie na vipaji mbalimbali” amesisitiza
Awali Mkurugenzi wa Sayansi Teknolojia na Ubunifu kutoka Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Maulilio Kipanyula amesema kuwa mafunzo hayo ni ya siku moja yenye lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao kwenda kuzitambua na kuziibua bunifu katika maeneo yao ya kazi.
Prof,Kipanyula amesema kuwa kupitia mafunzo hayo watayaainisha maeneo ambayo maafisa Maendeleo ya Jamii na Maafisa udhibiti ubora wa elimu wanatakiwa wakayafanyie kazi katika kuibua ubunifu na teknolojia mbalimbali.
“Lengo letu elimu ya Mafunzo haya ifike hadi ngazi za Wilaya na hadi kata na tutawapa elimu kupitia maada mbalimbali ambazo zitatolewa na COSTECH na SIDO ya kuwajengea uwezo” amesema Prof Kipanyula.