Home Mchanganyiko Mkirikiti Akutana na Mzigo wa Malalamiko ya Ardhi Mjini Babati

Mkirikiti Akutana na Mzigo wa Malalamiko ya Ardhi Mjini Babati

0

Na John Walter-Babati

Mkuu wa Mkoa wa Manyara Joseph Mkirikiti ameiagiza idara ya Ardhi Halmashauri  ya Mji wa Babati kuweka ratiba ya kusikiliza kero za wananchi na  kutatua migogoro ya ardhi  iliopo.

Amesema kwa kufanya hivyo itasaidia kwa kiwango kikubwa kujua chanzo cha migogoro hiyo na kuipatia ufumbuzi wa haraka.

Mkirikiti ametoa agizo hilo baada ya kupokea kero nyingi zinazohusu ardhi  wakati  alipofanya  mkutano na wananchi mjini hapo leo Agosti 24,2020.

Kwa upande mwingine amewataka wananchi wote  waliowasilisha malalamiko  na wenye  kero kufika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Babati agosti 28 mwaka huu kwa ajili ya ufumbuzi wa malalamiko na kero zao.

Hii ilikuwa ni ziara yake ya kwanza mjini Babati tangu aanze kuwatumikia wananchi hao mapema mwezi Julai akimpokea mtangulizi wake Alexender Mnyeti aliekwenda kugombea Ubunge jimbo la Misungwi mkoani Mwanza kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi.

Mapema Mkuu wa mkoa alizungumza na wafanyabiashara mkoani hapo na kusikiliza kero zinazowakabili hukuvakiwaahidi ushirikiano.