*********************************
LUDEWA
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe Agosti 22/2020 wamejitokeza kwa Wingi kumsindikiza Mgombea wa Ubunge Jimbo la Ludewa Wakili Joseph Zacharius Kamonga kwenda kuchukua FOMU ya kugombea nafasi hiyo kwenye Ofisi ya Msimamizi wa Uchaguzi Wilayani Ludewa.
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo hilo Ndg, Deo Ngalawa na Wagombea wengine wa CCM walioshiriki Mchakato wa Kura za Maoni wameshiriki Kikamilifu zoezi hilo na kuahidi kutoa Ushirikiano wa kutosha kwa Joseph Kamonga katika kipindi cha Kampeni ili Chama Cha Mapinduzi kiweze kushinda kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28/2020 hatimae Wananchi wa Ludewa waweze kupata Maendeleo.