Baadhi ya wanaCCM waliomsindikiza mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CCM Miraji Mtaturu.
Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akisalimiana na mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CCM Miraji Mtaturu kabla ya kumkabidhi fomu ya kugombea jimbo hilo.
Msimamizi wa uchaguzi wilaya ya Ikungi Justice Kijazi akimkabidhi fomu mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CCM Miraji Mtaturu.
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki Miraji Mtaturu akiwa na Mwenyekiti wa Ccm wilaya Mika Likapakapa
Mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya CCM Miraji Mtaturu akiwa pamoja na Wana CCM na viongozi wa CCM wilaya waliomsindikiza kuchukua fomu ya kugombea Jimbo hilo
……………………………………………………………………….
MAMIA ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Leo wamejitokeza kumsindikiza mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama hicho Miraji Mtaturu kwenda kuchukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) ya kuomba kuteuliwa kugombea nafasi hiyo.
Mtaturu ameenda kuchukua fomu hiyo ili kuomba kuteuliwa kwa kipindi kingine kuwa mgombea katika jimbo hilo ambapo Wana CCM hao walimsindikiza hadi nje ya ofisi za Tume hiyo zilizopo kwenye jengo la halmashauri ya Ikungi.
Akizungumza mara baada ya kuchukua fomu hiyo kutoka kwa msimamizi wa uchaguzi katika Jimbo hilo Justice Kijazi,Mtaturu ameahidi kufanya kampeni za kistaarabu Kama kanuni za uchaguzi zinavyoelekeza.
“Naomba niwahakikishie kwa niaba ya chama changu chenye nidhamu,taratibu na kinachozingatia maadili,tutafanya kampeni zetu kwa kistaarabu,tutaenda kunadi Sera zetu kwa sababu tunazo,
Amesema katika kampeni hizo watafuata miongozo na kuheshimu kanuni zote za uchaguzi zilizowekwa.
“Chama Cha Mapinduzi ni Chama Cha kistaarabu,Rais Dkt John Magufuli amefanya kazi kubwa katika uongozi wake hivyo ni nafasi yetu kupitia majukwaa ya kampeni kueleza alichofanya na kusema tutakachokifanya kupitia Ilani yetu,”alisema Mtaturu.
Amesema wanaamini uchaguzi utakwenda kwa amani na utamalizika vizuri.