Home Mchanganyiko MABEYO AONGOZA GWARIDE MAALUMU LA HESHIMA LA KUWAAGA MAAFISA WASTAAFU WA JESHI...

MABEYO AONGOZA GWARIDE MAALUMU LA HESHIMA LA KUWAAGA MAAFISA WASTAAFU WA JESHI NGAZI ZA JUU  

0

************************************

NA EMMANUEL MBATILO

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama (JWTZ), Venance Mabeyo ameongoza Gwaride maalumu la heshima la kuwaaga Maafisa 16 wa ngazi za juu wa Jeshi waliostaafu.

Gwaride hilo limefanyika leo jijini Dar es Salaam ambapo Luten Jenerali mmoja (1), Meja Jenerali Sita (6) na mabrigedia Jenerali tisa (9).

Nae Mmoja wa wastaafu, Luten Jenerali (Mstaafu), Paul Massao amesema kutumikia jeshi ni kazi ambayo ni yakujitolea inamuhitaji mtu aliekuwa mzarendo wa nchi yake na asiejali masrahi binafsi.

Aidha Massao amesema kuwa jeshi ni mali ya Wananchi hivyo wanatakiwa kutoa ushirikiano wakutosha ili kuweza kukabiliana na vita baridi ya vikundi vya watu wasiotakia mema Tanzania.

Kwa uapnde wake Brigedia Jenerali (Mstaafu), Mary Hiki amesema jeshi linamisingi na taratibu zake, ukizifuata utaishi muda mrefu jeshini na kustaafu kwa heshima.

Amesema katika siku hiyo yeye ni mwanamke pekee anaestaafu mwenye cheo kikubwa jeshini na anafurahi kumuacha mwanamke mwingine mwenye cheo cha juu.

Nae Brigedia Jenerali Hawa Kodi ambaye ni Kaimu Mkuu wa Ununuzi na Ugavi Jeshini amesema ni jambo la kipekee kwa mwenzake kupatiwa heshima hivyo ataendeleza mambo mazuri aliyoyafanya na kuenzi ili nae aweze kupatiwa heshima kama hiyo.