Home Mchanganyiko WAAJIRI NCHINI WASHAURIWA KUELEWA ZANA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

WAAJIRI NCHINI WASHAURIWA KUELEWA ZANA YA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI

0

Mtendaji mkuu wa OSHA Bi Khadija Mwenda akiwa na Mkurugenzi wa Usalama na Afya toka OSHA Mhandisi Alex Ngata. Mwenyekiti wa Boadi ya Ushauri ya OSHA, Dr. Adelhem Meru akiongea na Wanachama wa TCCIA Mkoa wa Morogoro.

 Mtendaji Mkuu wa OSHA, Bi Khadija Mwenda akiongea na Wanachama wa TCCIA Mkoa wa Morogoro( hawapo pichani) katika kikao kazi baina ya OSHA na TCCIA.

Mgeni rasmi Dr. Adlehem Meru akiwa pamoja na Viongozi mbalimbali wa OSHA pamoja na TCCIA mkoa wa Morogoro.

Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Watendaji wa  OSHA pamoja  taasisi na idara  zilizopo chini ya ofisi ya Ofisi ya Waziri mkuu Kazi, Vijana,Ajira na wenye Ulemavu.

**********************************

Mwandishi wetu, Morogoro

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi (OSHA) Dr Adelhem Meru, amewashauri waajiri nchini, kuielewa vizuri zana ya usalama na afya mahali pa kazi, na hivyo kuhakikisha wanalinda afya na usalama wa wafanyakazi wao, ili waweze kuzalisha kwa wingi na kufikia malengo waliojiwekea.

Kauli hiyo imetolewa mjini Morogoro wakati wa kikao kazi baina ya Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) pamoja na Chama cha Wafanyabiashara, Viwanda na Kilimo nchini (TCCIA) mkoani Morogoro kwenye kikao kazi ambacho pia kilikuwa na lengo la kuitambulisha kampeni ya vision zero mkoani Morogoro kampeni maalumu ambayo inalenga kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi. Dr.Meru amesema endapo waajiri hawatazingatia masuala ya usalama na afya, hawataweza kufikia malengo yao waliojiwekea ambao ni lengo kubwa la mfanyabiashara. Amesema hayo hayatawezekana endapo wafanyakazi hawatawekewa mazingira bora ya afya zao na usalama wao.
“Usalama na Afya mahali pa kazi ni nguzo muhimu katika uzalishaji, katika utoaji wa huduma mahali popote pale ukiwa na wafanyakazi ambao afya zao sio bora uzalishaji wao utakuwa sio bora, matokeo yake hata malengo yako kama mwajiri uliojiwekea yatakuwa sio bora. Hivyo na wahamasisha Waajiri wote kuielewe vizuri dhana ya usalama na afya kiuhalisia, tukitoka hapa tuende kuhamasishana wafanyakazi wetu wanakuwa katika mazingira ambayo ni salama na sio dhaifu,” Alisema Dr Meru
Dr.Meru amepongeza juhudi za Mhe Rais Dr. John Pombe Magufuli kwa kuweza kufikisha nchi kwenye uchumi wa kati hata kabla ya muda ambao ulikuwa umepangwa, amesema sera za nchi zilikuwa zinasema nchi itafikia uchumi wa kati ifikapo 2020/2025, amesema kutokana na uongozi shupavu wa Rais John Pombe Magufuli, amewezesha kufikia uchumi wa kati hata kabla ya muda uliopangwa,amesema wanachama wa TCCIA wana mchango mkubwa walioutoa katika kuifikisha nchi kwenye uchumi wa kati kwani, kufikia uchumi wa kati, kuna mchango mkubwa ambao wanachama wao wa TCCIA wameutoa.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali Pa Kazi, amesema waliona kuna umuhimu OSHA kushirikiana na TCCIA katika kuhakikisha wanashughulikia kero na changamoto za wafanyabiashara nchini, kwani mchango wao ni mkubwa katika kukuza uchumi wa nchi.

Amesema OSHA imetekeleza Andiko la Blue print kwa kiasi kikubwa kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji na ufanyabiashara nchini, kwa kuondoa tozo mbalimbali ambazo zilikuwa kikwazo kwa wawekezaji na wafanyabishara nchini.

Mwenda amesema OSHA kama taasisi wezeshi itaendelea kushirikiana na wadau kupitia vyama vyao ili kuweza kutatua changamoto zinazowakabili, amesema sekta ambayo sio rasmi inaajiri watu wengi sana, hivyo OSHA wataendelea kushirikiana na TCCIA katika kuhakisha sekta hii inaendelea kukua na kuchangia katika ukuaji wa uchumi.

Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa wa Morogoro ndugu Mwadhini Omari Myanza amesema ameishukuru OSHA kwa kutekeleza ipasavyo yale yote yalioelekezwa kwenye Blue Brint, na hivyo kuwasaidia wadau wao.

“OSHA ni chombo ambacho huwezi kukiweka pembeni katika mapinduzi ya viwanda, kwasababu kila mahali unapopiga hatua unahitaji kuwa na elimu ya usalama na afya wakati wa uzalishaji, kwa hotuba hii imetuzindua na kukumbuka kuwa serikali yetu imefanya mambo mengi, kwasababu mambo yote ambayo yaliyotolewa kwenye blue print , OSHA imejitahidi kuzingatia ushauri uliotolewa sasa tunaenda vizuri” alisema bwana Myanza.

Kwa upande wake,mmoja wa washiriki kwenye kikao hicho kutoka Flomi Hotel ya Mkoani Morogroro Bi Paulina Laizeri amesema Kikao hicho kimewasaidia na kuwajengea uelewa mpana zaidi masuala ambayo walikuwa hawayaelewi na hivyo yatawasaidia katika shughuli zao wanazozifanya kwa kuhakikisha mazingira ya wafanyakazi yanaboreshwa.

“OSHA imetusaidia sana kuboresha mazingira yetu ya kazi, na leo kupitia kikao hiki nimejifunza mengi kupitia michango mbalimbali ya wadau waliuokuwa wakiongea na kuchangia, na sasa ntaweza kutekeleza pale ambapo kidogo nilikuwa sielewi” alisema Bi Paulina.

Kikao kazi baina ya OSHA na wadau TCCIA mkoa wa Morogoro kiliandaliwa kwa lengo kuitambulisha kampeni ya vision zero, mpango maalumu wa kupunguza ajali na magonjwa sehemu za kazi, sambamba na kusikiliza kero mbalimbali ambazo ni kikwazo katika utekelezaji wa sheria ya usalama na afya mahali pa kazi, sheria na 5 ya mwaka 2003