Ofisa Elimu Taaluma Wilaya ya Nyasa Bw. Rainery Ngonyani akikagua mradi wa ujenzi wa vyoo vya kisasa katika Shule ya Msingi Ukuli na Lumeme katika Tarfa ya Mpepo Wilayani Nyasa Hivi karibuni.Vyoo hivi Vimeongeza mahudhurio na kupanda kwa Taaluma Wilayani Nyasa.
*******************************
Ujenzi wa Miundombinu ya Vyoo vya kisasa unaoendelea kujengwa Wilayani Nyasa, katika shule za msingi Umeongeza mahudhurio ya wanafunzi, yamepunguza ongezeko la magonjwa ya njia ya mkojo kwa watoto wa kike na kupanda kwa Taaluma.
Hayo yameelezwa hivi karibuni na baadhi ya walimu wakuu wa shule za Ukuli na Lumeme ambazo zinatekeleza miradi ya Ujenzi wa Vyoo, katika Tarafa ya Mpepo Wilayani hapa.
Walimu wakuu hao wamefafanua kuwa, kabla ya ujenzi wa miundombinu ya Vyoo mahudhurio yalikuwa ni wastani wa asilimia 95 kwa siku mara baada ya kujenga miundombinu mahudhurio yamepanda kufikia aslimia 98 kwa siku na wanafunzi wana ari ya kujifunza kwa kuwa shule ina miundombinu bora. Aidha wanafunzi wakike wengi walikosa masomo hasa wanapokuwa katika kipindi cha hedhi kutokana na vyoo vya awali kukosa faragha na usalama. Hali hii kwa sasa imetoweka kutoka nya vyoo bora vilivyojengwa.
Walimu wakuu hao wameipongeza Serikali ya Awamu ya Tano inayoongozwa na Dkt John Pombe Magufuli, kwa kuboresha miundombinu ya Vyoo, madarasa, na Nyumba za walimu. Uboreshaji huu wa miundombinu umeleta ari nzuri ya kufundisha kwa walimu na ujifunzaji rahisi kwa wanafunzi.
“Mradi huu wa vyoo vya kisasa umeongeza mahudhurio ya wanafunzi ambao awali walikuwa wakihudhuria kwa wastani wa asilimia 95 kwa siku, mara baada ya kujenga miundombinu hii mahudhurio yameongezeka kufikia asilimia 98 kwa siku, Nitoe Shukrani za dhati kwa Serikali ya Awamu ya 5 inayoongozwa na Rais Magufuli kwa Kuboresha Miundombinu ya Elimu hali inayo sababisha taaluma kupanda na utoro kutokomea”. Alisema Rhoda Mpangala mwl mkuu msaidizi wa Shule ya Ukuli.
Naye mwalimu faida Hyera wa shule ya Msingi Lumeme alisema awali walikuwa wakipata shida ya maji, wakati wakihitaji huduma ya vyoo vya shule, hali iliyokuwa ikisababisha wanafunzi kutafuta maji umbali mrefu lakini kwa sa sasa kero imeisha baada ya kuletewa mtandao wa maji na wanafunzi wanahudhuria wakiwa hawana wasiwasi kipindi wanapokuwa Shuleni hali iliyowafanya kuongeza ari ya kujifunza na kuhudhuria shuleni na kuacha utoro.
Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa inatekeleza miradi ya ujenzi wa vyoo vya kisasa katika shule saba za Msingi na jumla ya matundu 117 yanajengwa yanayogharimu tsh 175,778,504.97 , na zimepelekwa katika shule ya Msingi Likwilu (15,827,214.97) matundu kumi ya Vyoo na mfumo wa maji kwa shule zote,, Kuhamba (18,719,214.97) matundu 13, na Lumeme ni Tsh 19,547,214.97 matundu 11. Shule zingine zilizopewa fedha ni Liparamba (21,757,214.97) matundu 13, Ukuli 26,171,214.97 matundu 17, Kilosa47,625,214.97 matundu 36 na Mwongozo ni Tsh ( 26,131,214.97 , lengo la kuboresha miundombinu hii ni kuwafanya wanafunzi wavutiwe na mazingira ya kujifunzia hali ambayo itasaidia kupunguza utoro na kupandisha kiwango cha elimu Wilayani Nyasa.
Mratibu wa Ujenzi wa vyoo kupitia Mradi wa Swash Wilaya ya Nyasa Mwl Rainery Ngonyani amesema wananchi wa Wilaya ya Nyasa wameipokea miradi hiyo na kutekeleza kwa umakini wa hali ya juu kwa kuwa imelenga kutatua changamoto za wanafunzi kujifunza. Aidha wanafunzi wanafurahia miundombinu Bora iliyopo Mashuleni na wanajamii wanatakiwa kuitunza. Hata hivyo ameongeza kusema Vyoo hivi vinaenda kutatua kabisa changamoto ya watoto wa kike kukosa vipindi wakiwa katika Hedhi, kwa kuwa wasichana hao walikosa faragha na maji ya kutosha kwa ajili ya usafi binafsi wanapokuwa katika hali hiyo. Hata hivyo aliwasisitiza Walimu wakuu kuhahakisha vifaa vya hedhi salama vinakuwepo shuleni katika kipindi chote cha masomo na kuhakikisha vyoo vinakuwa salama daima.
Mkurugenzi Mtendaji Wilaya ya Nyasa Bw Jimson Mhagama akiwa anakagua ujenzi wa miradi hiyo amewata walimu wakuu, kamati za Shule na wananchi kuhakikisha wanashiriki kikamilifu katika utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwa ni mali yao na Serikali imetoa fedha hizo manufaa ya wanajamii walioko katika shule hizo.
Aidha bw Mhagama amemshukuru na kumpongeza Rais Dkt John Magufuli kwa kuijali na Kuikumbuka Wilaya ya Nyasa kwa kuipa fedha za kutekeleza miradi mbalimbali