Home Siasa MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI...

MWENYEKITI WA CCM RAIS DK. JOHN POMBE MAGUFULI AFUNGUA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CCM

0

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akifungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM kitakachoteua wagombea ubunge kupitia chama hicho unaotarajiwa kufanyika Oktoba 28 2020, Kikao hicho kinafanyika katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo.

(PICHA NA JOHN BUKUKU-FULLSHANGWE.DODOMA)

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiimba wimbo pamoja na viongozi wengine kabla ya kufungua kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM taifa. kitakachoteua wagombea ubunge kupitia chama hicho utakaofanyika Oktoba 28 2020 Kikao hicho kinafanyika  katika ukumbi wa White House jijini Dodoma leo, Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Rais Dk. Ali Mohamed Shein na kutoka kulia ni Mzee Philip Mangula Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara na Katibu Mkuu wa CCM Dk. Bashiru Ali.

MNEC wa mkoa wa Iringa Bw. Salim Ahmed Abri akipitia makabrasha ya kikao hicho na wajumbe wenzake kabla ya kuanza kwa kikao.

Wajumbe mbalimbali wakiwa wameketi ukumbini.