Home Mchanganyiko JKT YATANGAZA NAFASI ZA KUJITOLEA KWA VIJANA WA KITANZANIA

JKT YATANGAZA NAFASI ZA KUJITOLEA KWA VIJANA WA KITANZANIA

0

Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Julius Kadawi akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma wakati wa kutangaza nafasi za Kujitolea za JKT 2020. Badhi ya Waandishi wa Habari wakimfatilia kwa makini Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Julius Kadawi(hayupo pichani) wakati akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma . Mkuu wa Tawi la Utawala JKT, Kanali Julius Kadawi akizungumza na vyombo vya habari leo Jijini Dodoma wakati wa kutangaza nafasi za Kujitolea za JKT 2020.

Muonekano wa Majengo ya Mkao Makuu ya JKT yaliyoko Jijini Dodoma

………………………………………………………………

Na. Majid Abdulkarim, Dodoma.

Mkuu wa Jeshi la kujenga Taifa JKT Meja Jenerali Charles Mbuge ametangaza nafasi za kujiunga na mafunzo ya Jeshi hilo ya kujitolea kwa vijana wote wa Tanzania Bara na Visiwani kwa mwaka 2020.

Akitangaza nafasi hizo kupitia vyombo vya Habari jijini Dodoma Kwa niaba ya Mkuu wa Jeshi hilo, Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Kanali Julius Kadawi amesema utaratibu wa maandalizi ya vijana hao kwaajili ya kujiunga na Jeshi hilo unaanza mwezi Agost 2020.

“Uratibu wa Vijana kuomba na hatimaye kuchaguliwa kujiunga na mafunzo hayo, unaratibiwa na Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wilaya ambako mwombaji anaishi”, ameeleza Kanali Kadawi.

Hata hivyo Kanali Kadawi amesisitiza kuwa vijana watakaopata fursa hiyo watambue kuwa Jeshi la Kujenga Taifa halitoi ajira kwa vijana, halihusiki katika kuwatafutia ajira katika asasi , vyombo vya ulinzi na Usalama na mashirika mbalimbali ya Serikali na yasiyoyakiserikali, bali hutoa mafunzo ambayo yatawasaidia vijana kujiajiri wenyewe mara baada ya kumaliza Mkataba wao na Jeshi la Kujenga Taifa.

 Kanali Kadawi ameongeza kuwa kutokana na Ugonjwa wa Homa kali ya Mapafu (COVID-19) hapa Nchini, Tahadhari za kuzuia maambukizi ya ugonjwa huo kama ambavyo zimekuwa zikielekezwa na Serikali kupitia Wizara ya Afya zitazingatiwa katika kipindi chote ambacho vijana watakapokuwa kambini.