Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (Bara) Bw.Gerald Kusaya akiongea na watendaji wa mradi wa Kuimarisha Uzalishaji Mpunga (ERPP) alipokagua skimu ya umwagiliaji ya Mtwango wilaya ya Magharibi ‘B’ Zanzibar leo.Kulia kwake ni Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo( Zanzibar) Bi.Maryam Abdulla.Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya akizungumza na waandishi wa habari mjini kuhusu miradi inayotekelezwa na wizara yake kwa ushirikiano na Wizara ya Kilimo Zanzibar ikiwemo ya Kudhibiti Sumukuvu (TANIPAC) na Kuongeza Tija na uzalishaji zao la Mpunga (ERPP)
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo (Bara) Bw.Gerald Kusaya akikagua skimu ya umwagiliaji ya Mtwango wilaya ya Magharibi ‘B’ Zanzibar inayotekelezwa chini ya Mradi wa ERPP.
Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo ( Bara) Bw. Gerald Kusaya akionyesha kungua za gari wakati alipokabidhi gari hilo pamoja na pikipiki mbili kwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi Zanzibar Bi.Maryam Abdulla ( kulia) leo mjini Zanzibar.Gari hilo limetolewa kwa ajili ya uratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu upande wa Zanzibar.
Katibu Mkuu Kilimo ( Bara) Bw.Gerald Kusaya aliyevaa tai akiwa na Katibu Mkuu Kilimo (Zanzibar) Bi.Maryam Abdulla alivaa ushungi mwekundu wakiongea na wakulima wa zao la mpunga katika skimu ya Mtwango wilaya ya Magharibi ‘B’ Zanzibar .Katibu Mkuu huyo yuko ziarani Zanzibar kukagua miradi ya kilimo inayotekelezwa kwa pamoja na serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar leo
Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Sumukuvu nchini (TANIPAC) Clepin Josephat akitoa maelezo kwa Makatibu Wakuu wizara za Kilimo Bw.Gerald Kusaya ( aliyevaa tai) na Bi.Maryam Abdulla ( aliyevaa ushingi mwekundu) kuhusu eneo patakapojengwa ghala la kuhifadhia nafaka tani 1,500 katika eneo la Kizimbani Wilaya ya Magharibi ‘A’ Zanzibar leo.