**********************************
NA EMMANUEL MBATILO
Zikiwa zimebaki siku chache kuelekea mechi ya kirafiki kati ya Simba dhidi ya Vital’O ya nchini Burundi katika tamasha la Simba Day hapo Jumamosi ya wiki hii, inategemewa tamashahilo kuwa la aina yake.
Akizungumza na Wanahabari Jijini Dar es Salaam, kuelekea tamasha hilo, Msimaji wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema wanategemea kupata changamoto kubwa kwa timu hiyo ya Vital,O kwani wanauwezo mkubwa kiuchezaji.
“Tulipanga kucheza na Al Ahly lakini changamoto ya corona imefanya jambo hilo kuwa gumu. Tunaamini Vital’O itatupa changamoto nzuri kwenye mchezo huo”.Amesema Haji Manara.
Katika tamasha hilo ambalo linategemea kuwa l aina yake pia kutakuwa na buruani ya muziki kutoka kwa wasanii wakubwa mbalimbali wa hapa nchi.
“Simba Day burudani itatolewa na Twanga Pepeta, Tunda Man, Meja Kunta, Mwasiti na kipekee atakuwepo Diamond Platinumz. Litakuwa kama tamasha la mziki, amekusudia kufanya jambo kubwa na kwa kupitia hilo kesho alhamisi kutakuwa na BIG SURPRISE kwa Wanasimba. MC atakuwa Mpoki.” Amesema Haji Manara.