Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Albert Msovela akisoma barua ya utambulisho wa Maofisa kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa waliofika katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa huo leo kwa ajili ya kujitambulisha mkoani hapo na kuendelea na zoezi la ugawaji wa fomu za gharama za uchaguzi pamoja na kufuatilia mienendo ya vyama vya vya siasa wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020. Kutoka kushoto ni Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Fabian Kamoga, Mratibu wa Kikosi kazi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anayeratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Kanda ya Ziwa, kundi B, Bibi. Chevu Sepeku na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Bw. James. Kanda ya ziwa B inahusisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
Mratibu wa Kikosi kazi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anayeratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Kanda ya Ziwa, kundi B, Bibi. Chevu Sepeku akikabidhi fomu za gharama za uchaguzi kwa Mratibu wa Uchaguzi Mkoa wa Shinyanga Bw. Fabian Kamoga mara baada ya kujitambulisha katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa tayari kwa kuendelea na jukumu la kusambaza fomu hizo leo mjini Shinyanga. Zoezi hilo ni kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sheria ya gharama za uchaguzi na 6 ya mwaka 2010. Kanda hiyo inahusisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
Mratibu wa Kikosi kazi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anayeratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Kanda ya Ziwa, kundi B, Bibi. Chevu Sepeku akikabidhi fomu za gharama za uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Solwa,Bibi Hoja Mahiba leo wilayani Shinyanga. Zoezi hilo ni kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sheria ya gharama za uchaguzi na 6 ya mwaka 2010. Kanda hiyo inahusisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara.
Mratibu wa Kikosi kazi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anayeratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Kanda ya Ziwa, kundi B, Bibi. Chevu Sepeku akikabidhi fomu za gharama za uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Kahama Mjini, Anderson Msumba leo mjini Kahama. Zoezi hilo ni kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sheria ya gharama za uchaguzi na 6 ya mwaka 2010. Kanda hiyo inahusisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na MaraMratibu wa Kikosi kazi toka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa anayeratibu shughuli za Uchaguzi Mkuu mwaka 2020 Kanda ya Ziwa, kundi B, Bibi. Chevu Sepeku akikabidhi fomu za gharama za uchaguzi kwa Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Msalama, Simon Berege leo mjini Kahama. Zoezi hilo ni kurahisisha utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Msajili ambayo ndiyo yenye dhamana ya kusimamia sheria ya gharama za uchaguzi na 6 ya mwaka 2010. Kanda hiyo inahusisha mikoa ya Shinyanga, Simiyu na Mara