Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu maandalizi ya kuelekea tamasha kubwa la kuombea uchaguzi mkuu.
**********************************
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama amewataka watanzania kushiriki katika tamasha kubwa la kuombea uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu.
Tamasha hilo linatarajia kufanyika Juma pili ya mwezi Agost 23 mwaka huu katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, ambapo zaidi ya waimbaji 20 wa nyimbo injili watakuwepo akiwemo Rose Mohando, Christina Shusho, Chiristopher Mwangira, Bony Mwaitege pamoja na kwaya mbalimbali.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Msama, amesema kuwa wamejiandaa kwa ajili ya kufanya tamasha hilo ili kuombea uchanguzi mkuu ufanyike kwa amani na utulivu.
Bw. Msama amesema kuwa katika tamasha hilo watashiriki maaskofu kutoka madhehebu tofauti, viongozi wa serikali na taasisi kwa ajili kukusanyika pamoja na kuliombea taifa kufanya uchaguzi kwa amani.
“Tumepita katika mapito mbalimbali, watanzania tujitokeze tuungane pamoja katika kuliombea taifa ili uchaguzi mkuu ufanyike kwa amani na utulivu” amesema Bw. Msama.
Amefafanua kuwa tamasha hilo halitakuwa na kiingilio , kila mtu ataingia bure ili kumuomba mungu kwa pamoja kuelekea uchaguzi mkuu.
Bw. Msama ameeleza kuwa Maaskofu wa mazeebu mbalimbali, viongozi wa serikali na taasisi watashiriki siku, uku mwimbaji wa Rose Muhando ataweza kutambulisha nyimbo zake mpya katika tamasha hilo.