Mkurugenzi wa Mashtaka Bw. Biswalo Mganga amewaachia huru washtakiwa 25 siku ya jana waliokuwa wamewekwa katika gereza la Nzega mkoani Tabora, baada ya kutembelea gereza hilo na kujionea hali halisi ya uendeshaji na kusikiliza malalamiko ya washtakiwa hao.