



……………………………………………..
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, Angela Kairuki, akiongoza ujumbe wa maafisa kutoka wizara yake amefanya ziara ya kikazi katika kampuni ya Tanzania Distillers Limited (TDL) chini ya kampuni ya TBL Group katika eneo la Chang’ombe jijini Dar es Salaam na kujionea uzalishaji wa bidhaa zake na kusikiliza changamoto za uzalishaji na mafanikio ya kampuni na mchango wake katika kukuza uchumi wa taifa sambamba na mkakati wake wa kufanikisha ajenda ya serikali ya Tanzania ya viwanda.