Home Mchanganyiko WATU WANNE MIKONONI MWA POLISI MKOANI MWANZA

WATU WANNE MIKONONI MWA POLISI MKOANI MWANZA

0

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAWASHIKILIA
WATU WANNE KWA TUHUMA ZA MAKOSA MBALIMBALI
YA KIUHALIFU.
TUKIO LA KWANZA.
TAREHE 16.08.2020 MAJIRA YA 04:00HRS HUKO KATIKA KITONGOJI CHA KAYENZE B, KATA YA LUTALE, WILAYA YA MAGU,KUNDI LA WAHALIFU WALIIVUNJA NA KUIBA
KATIKA KANISA LA KKKT USHARIKA WA GENERETH, MARA BAADA YA TAARIFA HIYO KUPATIKANA POLISI MSAKO MKALI KWA KUSHIRIKIANA NA WANANCHI WA
ENEO HILO ULIFANYWA NA KUFANIKIWA KUPATA MALI ZILIZOIBWA AMBAZO NI POWER MIXER MOJA, GENERATOR MBILI AINA YA KING MAX 4500 NA KING MAX 5900, VITAMBAA 36 VYA MADHABAHUNI, BIBLIA MBILI, KITABU KIMOJA CHA NYIMBO ZA DINI, CD 6 ZA
MAHUBIRI, MICROPHONE 7, PAMOJA NA NYAYA ZAKE, STABILIZER MOJA NA COUNTER BOOK TATU ZA KUMBUKUMBU ZA KANISA . BIBLIA MOJA NA KITABU CHA

NYIMBO HADI SASA BADO HAVIJAPATIKANA. JESHI LIMEAPA KILA ALIYESHIRIKI WIZI HUO LAZIMA AKAMATWE, AIDHA WATUHUMIWA WAWILI WANASHIKILIWA NA POLISI KUSAIDIA UPELELEZI NA WATAFIKISHWA MAHAKAMANI HARAKA IWEZEKANAVYO
UPELELEZI UKIKAMILIKA.

TUKIO LA PILI.
TAREHE 16.08.2020 MAJIRA YA 09:00HRS HUKO KITONGOJI CHA MWABUGA, KIJIJI CHA MANAWA, KATA YA MISASI, WILAYANI MISUNGWI, JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA
LIMEFANIKIWA KUMKAMATA WILLIAM CHARLES, MIAKA 37, MSUKUMA, MKAZI WA MANAWA, KWA TUHUMA ZA KUMUUA MKEWE AITWAYE DOTTO MANONI, MIAKA 35,
MSUKUMA, MKULIMA, MKAZI WA MANAWA, KWA KUMKATA NA KITU CHENYE NCHA KALI KIDHANIWACHO KUWA NI PANGA KICHWANI NA KWENYE SHAVU LA KULIA
UCHUNGUZI WA AWALI WA MAUAJI HAYO YA KINYAMA NI MADAI YA MTUHUMIWA KUWA ALIMKUTA MKEWE AKIFANYA MAPENZI NA MWANAUME MWINGINE CHUMBANI KWAKE. JESHI LA POLISI HALIVUMILII WALA KUTOA FURSA YA VITENDO HIVYO IKIWA NI PAMOJA NA SABABU ZA KIKATILI ZINAZOTOLEWA NA MUHUSIKA NA ATAFIKISHWA MAHAKAMANI KUKABILIANA NA MKONO WA SHERIA HARAKA IWEZEKANAVYO

MWILI WA MAREHEMU TAYARI UMEFANYIWA UCHUNGUZI NA DAKTARI NA KUKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.

TUKIO LA TATU.
JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KUANZIA TAREHE 04.07.2020 HADI TAREHE 16. 08.2020, LIMEKAMATA MAGARI 33 YENYE VING’ORA, VIMULIMULI, TAA ZENYE MWANGA MKALI (SPOT LIGHT) NA TAA ZENYE KUWAKAWAKA KWA

KUBADILISHA RANGI ZINAZOWEKWA MBELE AMBAZO NI KERO KWA WATUMIAJI WENGINE WA BARABARA NA NIKINYUME NA SHERIA YA USALAMA BARABARANI, KWA
MUJIBU WA SHERIA ZA NCHI MAGARI YA VIONGOZI WAKUU WA NCHI AKIWEMO AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA, MAKAMU WA RAIS, RAIS WA
ZANZIBAR, WAZIRI MKUU NA VIONGIOZI WENGINE MASHUHURI WENYE HADHI ZINAZOSTAHIKI NA KUTAMBULIWA NA SHERIA PAMOJA NA MAGARI YA DHARURA KAMA YA POLISI, JESHI LA WANANCHI WA TANZANIA, ZIMAMOTO NA UOKOAJI, NA YALE YA KUBEBA WAGONJWA NDIO YANAYORUHUSIWA KUFUNGWA VIFAA
HIVYO.
HATA HIVYO MAGARI MENGINE YOTE AMBAYO HAYAJAAINISHWA KISHERIA HAYARUSIWI KUFUNGWA NA KUTUMIA VIFAA HIVYO. JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA NA ZOEZI LA KUWAFUATILIA NA KUWAKAMATA WALE WOTE WALIOFUNGA VIFAA HIVYO NA TAA PASIPOKUWA NA MAMLAKA YANAYOWASTAHILI.

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA LINAENDELEA KUWASHUKURU WANANCHI KWA USHIRIKIANO MZURI. PIA KUSISITIZA WASIFUMBIE MACHO VITENDO VYA UHALIFU
BALI WAENDELEE KUTOA TAARIFA ILI ZIWEZE KUFANYIWA KAZI NA MWANZA IENDELEE KUWA SALAMA..
IMETOLEWA NA;
Muliro JUMANNE MULIRO – ACP KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

17 AUGUST, 2020