Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI ), Mhe. Selemani Jafo akizungumza WAKATI alipofanya ziara katika hospiatali YA Uhuruinayojengwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Mhandisi wa SUMAJKT, Omari Kabalagu akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI ), Mhe. Selemani Jafo (kushoto)alipofanya ziara katika hospiatali ya Uhuru inayojengwa Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma.
Muonekano wa Hospitali ya Uhuru inayojengwa katika Wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma
……………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Dodoma
Serikali yalidhishwa na kasi ya ujenzi wa hospitali ya Uhuru inayojengwa wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Kauli hiyo imebainishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI ), Mhe. Selemani Jafo alipofanya ziara katika hospiatali hiyo ili kukagua maendeleo ya ujenzi huo.
Mhe. Jafo amesema kuwa sasa Hospiatali ya Uhuru inaonekana kwa macho na kivutio katika barabara ya Dodoma kwenda Morogoro.
Aidha Jafo amemtaka mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino Ndugu Athumani Masasi kuwafikishia mafundi wa SUMA JKT vifaa vinavyohitajika ili wawezekukamilisha ujenzi huo kwa wakati.
“Naomba niwambie kuwa nitawashangaa kuona mnaagiza tiilizi nje ya Nchi wakati hivi karibuni Mhe. Rais Magufuli amezindua kiwanda cha tailizi mkoani pwani.”, amesema Mhe. Jafo.
Pia Mhe. Jafo ameelekeza kuwa miradi yote ya TAMISEMMI inayotekelezwa inatakiwa kutumia vifaa vya ndani ya nchi ili kuendelea kukuza uchumi wa taifa na kama kutakuwa na ulazima ndo vifaa vinunuliwe nje ya Nchi.
Naye Mhandisi wa SUMAJKT Omari Kabalagu amesema kuwa walitarajia kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo Agusti 23 Mwaka huu, lakini kutokana na changamoto ya vifaa kutofika kwa wakati inalazimika kutokamilisha kwa muda uliopangwa.
“Hivyo kwa wakati hu vifaa vikifika kwa wakati basi ndani ya wiki nne tutakuwa tumekamilisha ujenzi huu na kukabdhi mradi huu kwenu”amesisitiza Mhandisi Kabalagu
Mhandisi Kabalagu amesema kuwa hivi sasa wamebakiza maeneo machache sana kukamilisha ujenzi huo ambayo ni mfumo wa maji, mfumo wa umeme, kuweka tailizi na leo wanaanza kuweka bati.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Wilaya ya Chamwino, Athmani Masasi amesema kuwa changamoto ilikuwa kwa wazabuni walichelewa kuleta viafaa lakini kwa sasa kila kitu kimekamilika na juma lijalo vivaa vyote vitakuwa saiti.