Home Michezo Ngumi kuchapwa Babati kitaifa,Mikwara Yaanza

Ngumi kuchapwa Babati kitaifa,Mikwara Yaanza

0

…………………………………………………….

Na John Walter-Babati
Kuelekea mashindano ya ngumi  kitaifa katika wilaya ya Babati, Mkuu wa wilaya hiyo, Lazaro Twanga amewaomba wadau wa Michezo kujitokeza kuddamini ili kufanikisha.

Akizungumza na wadau hao wakati wa mashindano ya utangulizi mjini  Babati Agosti 15, amesema ni wakati wa wadau Michezo mkoani manyara kujitokeza na kuonyesha kwa vitendo mapenzi waliyonayo katika kukuza Michezo mkoani hapo.

Jumla ya mabondia 23 wa mkoa wa Manyara wameonyesha utayari wa  kupambana kwenye mashindano hayo ya masumbwi yaliyopangwa kufanyika kitaifa  mkoani Manyara  septemba 6-12 mwaka huu Uwanja wa kwaraa mjini Babati.

Afisa Michezo Mkoa wa Manyara Charles Maguzu amesema timu za majeshi nazo  zitashirikia mashindano hayo yanayosubiriwa kwa hamu kubwa kanda hii ya kaskazini.

Mwenyekiti wa kamati ya mashindano hayo Niko Mwaibale amesema Maandalizi yanaendelea vyema na kwamba  wamejipanga  kuhakikisha mashindano hayo yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu ili kufikia lengo la kupata timu ya ambayo itashiriki mashindano  kitaifa.

Mabondia kutoka mkoa wa Manyara ni Issa Hussein, Charles John, Christian Charles, Ally Issa, Kide  Hamad, Kurwa  Abbas, Sefu Issa, Peter Niko, Jonas John, Amani Furaisha, Rashid Mbongwa, Steven Anastazi, Abrahamani Mnimbo, Abrahamani Ally, Dandi Vita,John Yomba,Tadey Sangoma, Ibrahimu Wegoro,Narisisi Miaga, Enos Erasro, Adamu Hassani, Pius George.