Home Mchanganyiko Mvomero wakaribisha wadau USMJ

Mvomero wakaribisha wadau USMJ

0
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hassani Njama akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea Halmashauri hiyo kujionea maendeleo ya Mradi wa Utunzaji Shirikishi wa misitu na uvunaji wa mkaa endelevu  kwa  manufaa ya wanavijiji.
(PICHA NA JOHN BUKUKU- MVOMERO)
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hassani Njama akipokea majarida na vipeperushi mbalimbali kutoka kwa Bi. Elida Fundi Afisa Uragbishi wa Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Jamii Tanzania (TFCG).
Bi. Elida Fundi Afisa Uragbishi wa Mradi wa (CoForEST) (Uhifadhi wa Misitu na biashara endelevu ya mazao ya misitu) unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC) akimpa maelezo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero Bw. Hassan Njama kuhusu mkakati wa utunzaji shirikishi wa misitu na mkaa endelevu.
Bi. Elida Fundi Afisa Uragibishi wa Mradi wa (CoForEST) Uhifadhi wa Misitu na boashara endelevu ya mazao ya misitu) unafadhiliwa na Shirika la Maendeleo na Ushirikiano la Uswisi (SDC)akimpa maelezo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mvomero Bw. Hassan Njama kuhusu mkakati wa utunzaji shirikishi wa misitu na mkaa endelevu kushoto ni Ofisa Misitu wilaya ya Mvomero Edward Kimweri.
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hassani Njama akimsikiliza Ofisa Misitu wilaya ya Mvomero Edward Kimweri wakati alipokuwa akitolea ufafanuzi baadhi ya mambo kuhusu utunzaji shirikishi wa misitu.
Bettie Luwuge Mkuu wa mawasiliano kutoka shirika la Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Jamii Tanzania (TFCG)
Muonekano wa jengo la Halmashauri ya wilaya ya Mvomero linavyoonekana katika picha.
……………………………………………….
Na Suleiman Msuya
HALMASHAURI ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro, imewakatibusha wadau mbalimbali wa uhifadhi wa mazingira na misitu ili waweze kushirikiana pamoja kutoa elimu ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu ya Jamii (USMJ).
Ukaribisho huo umetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Hassani Njama wakati akizungumza na waandishi wa habari waliomtembelea hivi karibuni ili kujua namna halmashauri yake inasimamia dhana ya USMJ.
Njama alisema Mvomero ni moja ya wilaya ambayo bado ina changamoto za uhifadhi hivyo anaamini iwapo wadau wengine watajitokeza na kushiriana na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Jamii Tanzania (TFCG) na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) changamoto hiyo itaisha.
“Nitumie nafasi hii kuwakaribisha wadau wa kama TFCG na MJUMITA ambao kupitia mradi wa Kuleta Mageuzi katika Sekta ya Mkaa Tanzania (TTCS) chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC), wameweza kutusaidi USMJ ambayo ilikuwa hati hati kupotea.
Tuna vijiji 10 hivyo lengo letu ni Kuongeza vijiji vingine vipya kwani manufaa yapo ni imani yangu kuwa katika bajeti ya 2020/2021 tunaweza kuanza,” alisema.
Njama alisema mkakati wao mkubwa pamoja na kuomba wadau wengine watahakikisha wanatoa elimu kwa wanavijiji ambao wanamiliki misitu ya vijiji pamoja na viongozi ili kila mmoja awe balozi wa USMJ.
Alisema USMJ katika wilaya yao itatekelezeka kwa urahisi kutokana na vijiji 101 kati 167 kuwa na mpango wa matumizi bora ya ardhi.
Aidha, Njama alitoa rai wa taasisi na mashirika ambayo yanajihusisha na mpango wa matumizi bora ya ardhi kusimamia mchakato huo hadi ufike mwisho ili jamii inufaike.
Ofisa Misitu wilaya ya Mvomero Edward Kimweri alisema mradi wa TTCS umechochea maendeleo na uhifadhi kwa kiwango kikubwa hivyo wao wataendelea kuungana na wadau wengine ambao wanahitaji kushirikiana.
Alisema jamii ambayo ina misitu ya asili na ile ya Serikali kuu imekuwa mwalimu mzuri katika kulinda na sababu kubwa ni kutokana na manufaa ambayo wanayaona.
“Kusema ukweli mradi huu wa TTCS umeturahisishia kazi sana sisi watumishi wa sekta ya misitu kwani tumekuwa na mabalozi wengi pale ambapo hali ya uharibifu inatokea naungana na ombi la mkurugenzi kuwakaribisha wadau wengine,” alisema.
Alisema vijiji ambayo vipo kwenye mradi vimekuwa na mipango mingi ya maendeleo jambo ambalo tunataka kulisambaza kwa vijiji vingine.
Aidha, akizungumzia tangazo la Serikali GN 417 Ofisa Misitu huyo alisema kwa mtazamo wake anaona ina faida na hasara hivyo kinachotakiwa ni watu wote wajipange kukabiliana nayo kwa maslahi ya misitu.
Kwa upande wake Ofisa Sera na Majadiliono kutoka MJUMITA, Elida Fundi alimueleza sababu ya wao kujikita katika USMJ ni kuhakikisha rasilimali misitu na mazingira yanakuwa salama kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
Alisema mradi wa TTCS umefikia kikomo Novemba 2019 lakini wamekuja na mradi mwingine ambao utajikita katika mafunzo kwa ngazi zote.
“Kwa takribani miaka nane tumekuwa tukitekeleza mradi wa TTCS, ila kwa sasa tumekuja na Mradi wa Kuhifadhi, Misitu kwa Kuwezesha Biashara Endelevu ya Mazao ya Misitu Tanzania (CoForEST) ni imani yangu tutaenda pamoja ili misitu yetu iwe salama na endelevu,” alisema.