Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza Agosti 14,2020 katika ofisi ya mkoa wa Njombe alipokua katika ziara ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na Wadau wa Sekta ya Habari mkoani hapo.
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Mhandisi Marwa Mwita Rubirya akizungumza wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na Wadau wa Sekta ya Habari mkoani hapo
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bibi.Upendo Mbelle akitoa maelezo kuhusu hali ya usikivu wa redio za shirika hilo ambapo amesema unaendelea kuimarika, ameysema hayo katika ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na Wadau wa Sekta ya Habari mkoani hapo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Uplands redio (Redio Njombe) mkoa wa Njombe alipokua katika ziara ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na Wadau wa Sekta ya Habari mkoani hapo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na Wadau wa Sekta ya Habari Agosti 14,2020 katika ofisi ya mkoa wa Njombe alipokua katika ziara ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na wadau hao.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe mkoa wa Njombe Bibi Ruth Msafiri akizumgumza wakati wa ziara ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) ya kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na Wadau wa Sekta ya Habari mkoani hapo.
…………………………………………………………………
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, NJOMBE
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe
amevipongeza Vyombo vya Habari vya binafsi ambavyo vinatoa habari zilichokatwa
kwa weledi na kuzingatia kaanuni na maadili ya uandishi wa habari.
Waziri Mwakyembe ameyasema hayo Agosti 14, 2020 mkoani Njombe katika ziara ya
kukagua usikivu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pamoja na kuzungumza na
Wadau wa Sekta ya Habari ambapo amesema kuwa vyombo vya habari vya binafsi
vimesaidia wananchi kupata habari hasa katika maeneo ambayo TBC imekua na
changamoto ya usikivu.
“Navipongeza vyombo vya habari vya binafsi kwa kuhabarisha umma mambo
mbalimbali yanayotekelezwa na Serikali pamoja na kuibua changamoto zinazowakabili
wananchi ambazo Serikali inazitatua, Ni vizuri kuendelea kufanya hivyo hasa katika
kipindi hiki cha uchaguzi wananchi wanatakiwa wafahamu sera za vyama mbalimbali
na utekelezaji uliofanywa na chama kilichopo madarakani ili waweze kuchagua
viongozi ambao ni sahihi” alisema, Dkt. Mwakyembe.
Dkt.Mwakyembe ameongeza kuwa wanahabari wanapaswa kutafuta,kuchakata na
kutoa habari sahihi kwa kuwa ni takwa la Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016
ambayo inasisitiza weledi na uhakika katika taaluma hiyo.
Akizungumzia Sekta ya Michezo Mhe Waziri Mwakyembe amesisitiza kuwa kanuni za
kusajili wachezaji wa kigeni hapa nchini alizoagiza Baraza la Michezo la Taifa (BMT)
wazianishe ikiwemo mchezaji kucheza timu ya Taifa analotoka, kushiriki ligi kuu ya
nchi yake pamoja na angalau kushiriki daraja la kwanza kwa zile nchi ambazo ziko
katika kundi la hamsini bora ya Shirikikisho la Soka Duniani (FIFA).
Aidha, Mhe.Mwakyembe amesema kuwa kila mwaka Serikali inatenga takriban Shilingi
Bilioni 3 kwa ajili ya michezo ya UMISETA na UMITASHUMTA hivyo ni jukumu la
waalimu wa vilabu hapa nchini kutafuta wachezaji kupitia mashindano hayo kwakua
vijana wanaoshiriki mashindano hayo wana uwezo, na itasaidia kukuza vipaji vya
vijana hao kuliko kuweka nguvu katika wachezaji wa nje.
Kwa upande wake Mhandisi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bibi. Upendo
Mbelle ameeleza kuwa shirika hilo linaendelea kuimarisha usikivu katika mkoa huo wa
Njombe ambapo amesema taratibu za manunuzi ya mtambo kwa ajili ya Mji wa
Njombe yamekamilika hivyo ndani ya muda mfupi ujao mji huo TBC Taifa na TBC FM
zitasikika vizuri.
“Kupitia fedha za Mfuko wa Mawasiliano kwa wote, Shirika litafunga mitambo maeneo
ya Ludewa na Makete ambapo tayari maeneo ya kusimika mitambo hiyo
yamepatikana, Hivyo kufikia mwisho wa mwaka wa fedha 2020/2021 usikivu utakuwa
umeimarika” alisema Bibi Upendo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe.Eng. Marwa Mwita Rubirya amesema wananchi
wana imani kubwa na chombo cha habari cha umma hivyo ni vizuri kikasikia maeneo
yote, huku akiwataka wanahabari kutumia lugha sahihi ya Kiswahili katika kuandika na
kutangaza habari na vipindi mbalimbali pamoja na kufanya utafiti katika jambo
ambalo wanataka kuhabarisha umma ili kuepuka kutoa habari zisizo sahihi.
Naye Mwakilishi wa Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Njombe Bw.Hamis Kasaki
ameishukuru Wizara kwa kukutana na wanahabari hao kujua changamoto
wanazokutana nazo katika maeneo yao ya kazi na kuzitatua ,ambapo wameahidi
kuendelea kufanya kazi hiyo kwa kufuata misingi na kanuni za taaluma hiyo.