********************************
NJOMBE
Kijana Shedrack Kihombo(29) mkazi wa kijiji cha Isindagosi kilichopo kata ya Itulahumba wilayani Wanging’ombe mkoani Njombe ambaye aligongwa na gari 2015 na kuvunjika na kisha sehemu yote ya chini ikiwemo miguu kupoteza mawasiliano amewaomba watanzania kumsaidia kwa hali na mali ili aweze kupatiwa matibabu katika hospitali ya viungo ya Inuka iliyopo wilayani humo ama kupata matibabu Muhimbili.
Kijana Shedrack amefikia hatua hiyo baada ya kutaabika kwa zaidi ya miaka mitano kitandani huku akiwa ametumia kila aina ya dawa bila mafanikio lakini matumaini yalianza kurejea baada ya kwenda hospitali ya Ikonda ambako alishauriwa kuanza kwanza na matibabu ya mazoezi ya viungo ndiyo mishipa iamke ili kufanyiwa usuaji jambo ambalo limemuwia gumu na kurejea kwa watanzania kuomba msaada.
Anasema hana tena uwezo wa kuamka na kutembea tena na amekuwa mtu wa kulazwa na kuamshwa na wakati mwingine anapokosa msaada mvua na jua ni lake.
Tangu apate ajali jijini Arusha na kurejea nyumbani Njombe Mama mzazi Leah Msangi na Nikson Kihombo hawakuwahi kukata tamaa ya kuokoa maisha ya kijana wao na Wakati mwingine wanalazimika kuuza mifugo, mashamba na mali zao nyingine hatua ambayo imewafanya kubaki masikini hadi sasa na kuwarudi kwa wasamalia wema.
Nae Nikson Muhogofi maarufu mwendambinguni ambaye ni mlemavu wa macho na mmoja wa viongozi wa vijana wenye ulemavu mkoani wa Njombe maisha ya shida na taabu anayoishi kijana Shedrack akaona umihimu wa kuanza kupigania afya yake ili arejee katika uzima wa awali huku akimtaja miraji yao kama hitaji lake namba moja.
Kumchangia chochote kufanikisha matibabu
tuma kwenda namba
0756811804
0712989477 jina leah msangi