Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakymbe
akizungumza na Uongozi wa Mkoa wa Ruvuma pamoja na Mhandisi Mkuu wa Shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) Bibi. Upendo Mbelle (alievaa sweta) wakati Waziri huyo
alipotembelea mitambo ya shirika hilo iliyopo Matogolo mkoani Ruvuma mnamo Agosti
13, 2020 ambapo amepongeza shirika hilo kwa kuimarisha usikivu katika Nyanda za
juu kusini.
Mhandisi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Bibi Upendo Mbelle
akizungumzia usikivu wa redio TBC Taifa na TBC FM katika mikoa ya Nyanda za juu
kusini ambapo amesema usikivu umeimarika, ameyasema hayo katika ziara ya Waziri
wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakymbe katika mitambo ya
shirika hilo iliyopo Matogolo mnamo
Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw.Pololet Mgema akizungumza wakati wa ziara ya
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakymbe (kulia)
wilayani hapo ya kukagua usikivu wa wa redio TBC Taifa na TBC FM katika mikoa ya
Nyanda za juu kusini
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakymbe
akifanya mahojiano na kituo cha redio cha Jogoo FM kilichopo Songea mkoani Ruvuma
ambapo amesisitiza weledi katika taaluma ya habari pamoja na wanahabari kuchakata
habari kwa usahihi.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakymbe
akizungumza na Wadau wa Habari mkoani Ruvuma alipofanya mkutano na wadau hao
ambapo amesisitiza ifikapo mwaka 2021 itakuwa mwisho kwa wanahabari wasiokua na
vigezo vilivyoanishwa katika Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakymbe
akisalimiana na mchezaji wa zamani wa timu za Majimaji, Simba na Timu ya Taifa Bw.
Steven Mapunda “Garicha” katika mkutano na wadau wa sekta anazozisimamia
mnamo Agosti 13,2020. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Songea Bw. Pololet Mgema.
………………………………………………………………….
Na Shamimu Nyaki – WHUSM, Songea
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ametoa
pongezi kwa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) kwa kuimarisha usikivu wa redio TBC
Taifa na TBC FM katika mikoa ya Nyanda za juu Kusini.
Waziri Mwakyembe ametoa pongezi hizo Agosti 13,202 alipotembelea mitambo ya
shirika hilo iliyopo Matogolo wilayani Songea mkoani Ruvuma ambapo amesema kuwa
nyanda za juu kusini ni eneo ambalo lina miinuko na mabonde ambayo huleta
changamoto ya uskivu kwa masafa ya FM changamoto hiyo imetatuliwa baada ya
mitambo kuwekwa kwenye mwinuko mkubwa.
“Nawapongeza sana TBC kwa uwekezaji huu ambao mmeufanya katika eneo hili,
umesaidia wananchi kupata habari kwa wakati kutoka katika chombo cha umma
ambacho ndio kunaaminika katika utoaji wa habari sahihi” alisema, Dkt. Mwakymbe.
Dkt. Mwakymbe ameongeza kuwa suala la miundombinu katika maeneo iliposimikwa
mitambo ni changamoto ambayo inatakiwa kutafutiwa ufumbuzi wa haraka ili
kurahisha huduma na zinazotolewa katika maeneo hayo,hivyo suala hilo ataliwasilisha
katika ngazi ya juu Serikalini.
Kwa upande wake Mhandisi Mkuu wa shirika hilo Bibi.Upendo Mbelle amesema kuwa,
mitambo huo ni wa kilo wati moja (KW 1) ambao uwezo wake wa kurusha matangazo
ni wa kiwango cha juu, huku akieleza kuwa lengo la TBC ni kuhakikisha maeneo yote
yenye changamoto ya usikivu yanashughulikiwa ikwemo kununua vipuri na kufanya
matengenezo kwa mitambo ambayo imechakaa.
“Mtambo huu ni miongoni mwa mitambo 60 iliyofungwa nchi zima ambayo inasaidia
redio za shirika kusikia, na katika eneo hili la Matogolo limesaidia maeneo ya Nyasa,
Mbambabay, Tunduru ambayo yalikua na usikivu hafifu kuimarika” alisema
Bibi.Upendo.
Katika hatua nyingine Waziri huyo amefanya mkutano na Wadau wa Habari wa mkoa
huo ambapo amewataka kuzingatia weledi katika taaluma ya habari ikiwemo
kuandika habari zenye ukweli,zilichokatwa vizuri ambazo zitasaidia jamii kuelewa
mambo mbalimbali ya nchi.
Dkt.Mwakyembe pia amesisitiza kuwa ifikapo mwaka 2021 hakuna Mwandishi wa
Habari yoyote ambaye atakuwa hajakidhi vigezo vya Sheria ya Huduma ya Habari ya
mwaka 2016 pamoja na kanuni zake za mwaka 2017, hataruhusiwa kufanya kazi ya
uandishi wa habari.
“Mwanahabari ni mwalimu, mkalimani, mfasili, mchambuzi hivyo ni lazima aheshimike
na kulindwa kama ajira zingine. Lakini pia mwanahabri anapaswa kutambua kuwa
hakuna uhuru wa habari usiokuwa na mipaka” alisisitiza Dkt.Mwakyembe.
Vile vile Mhe Waziri amewataka viongozi kutoa habari kwa wananchi zinazoelezea
utekelezaji katika maeneo hayo ili wananchi wafahamu serikali imeafanya nini,huku
akisistiza matumizi ya Kitambulisho cha wanahabri popote wanapokuwa wanatimiza
majuku yao.
Hata hivyo Waziri Mwakyembe alitembelea Makumbusho ya Majimaji Songea ambayo
yana kumbukumbu ya mashujaa waliopigania uhuru kutoka kwa wajerumani katika
vita ya Majimaji ya mwaka 1906 hadi 1907 ambapo amepongeza namna historia
ilivyohifadhiwa katika eneo hilo ambalo ni kivutio cha utalii wa kiutamaduni pamoja
na mali kale.