Home Mchanganyiko WAKAZI WA MPWAPWA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO ILI KUUNGANISHIWA UMEME

WAKAZI WA MPWAPWA WATAKIWA KUTOA USHIRIKIANO ILI KUUNGANISHIWA UMEME

0

 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Maza , kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma, wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa usambazaji umeme vijijini

Wananchi wa Kijiji cha Mazae  kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Nishati Subira Mgalu(hayupo pichani) wakati akiwa kwenye ziara ya kazi ya ukaguzi wa usambazaji umeme vijijini 

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu akifurahi mara baada ya kukata utepe kuashiri kuwashwa kwa umeme katika Kijiji cha Mazae kilichopo katika kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa,Mkoani Dodoma

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(mwenye kilemba) akiwa pamoja na walimu na wanafunzi wa shule ya Msingi Mazae iliyopo katika  Kijiji cha Mazae kilichopo katika kata ya Mazae, Wilaya ya Mpwapwa, Mkoani Dodoma mara baada ya kuwasha umeme katika shule hiyo

Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu(mwenye kilemba) akiwa pamoja na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Morogoro wakiwa katika ziara ya ukaguzi wa kazi ya usambazaji umeme katika maeneo mbalimbali ya  Kijiji cha Lumuma,kata ya Lumuma, Wilaya ya Kilosa, Mkoani Morogoro.

…………………………………………………………..
Na. Alex Sonna, Mpwapwa
Viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wilayani Mpwapwa wametakiwa kufanya kufanya uhamasishaji kwa wananchi wao kutoa ushirikiano kwa mkandarasi ili kuweza kuunganishiwa umeme kabla ya muda wa kutekeleza mradi haujaisha.
Wito huo umetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Subira Mgalu,alipokuwa akiwasha umeme katika maeneo ya Mazae,Kimagai na Lumuma pamoja na kuaangalia utekelezaji wa miradi mbalimbali katika wilaya hiyo.
Aidha amewataka wanachi wa wilaya hiyo kulipia kiasi cha 27000 ili kuweza kuunganishiwa umeme kwani mkandarasi yuko tayari kuwaunganishia ila wao hawajalipia gharama za kuunganishiwa.
“Kasi ya mkandarasi anapimwa kupitia idadi ya wananchi waliopatiwa huduma na sio kwa kutandaza nguzo mtaaani hivyo mpeni ushirikiano kwa kulipia gharama za umeme ili muweze kuunganishiwa na kundelea na maendeleo mengine.
Hivyo basi wanachi changamkieni fursa hiyo Wateja hawajalipia haraka sana kwani mkandarasi yuko tayari na gharama ni 27,0000 na mkilipia anaunga umeme.
Baada ya wiki mbili narudi hapa kuangalia kama mtakuwa mmetoa ushirikiano kwa mkandarasi ili wakati anamaliza muda wake tayari mmeunganishiwa umeme”, ameeleza Mgalu

Kwa upande wake mwanakijiji hicho Bw.Hamis Israel ametoa shukrani kwa Serikali chini ya Rais Dkt.Magufuli  kwa kuwapelekea huduma ya umeme katika kijiji chao na kuitaka Serikali kuondoa changamoto wanazozipata wananchi wakati akiwa wanahitaji huduma hiyo.

Katika ziara yake hiyo Naibu Waziri wa nishati pia alikagua kazi ya usambazaji umeme Mkoani Morogoro katika wilaya ya Kilosa na kuwashaa umeme katika kijiji cha lumuma kilichopo katika kata ya Lumuma na baadae kugagua umeme katika nyumba na maeneo ya biashara ambayo tayari wamewapelekewa umeme.