
Timu ya soka ya waandishi wa habari michezo nchini (Taswa SC) kesho Jumamosi Agosti 15 itacheza mechi maalum katika bonanza la Ujirani Mwema lililoandaliwa na Gereza za Wazo Hill.
Mecgi hiyo imepangwa kuanza saa 10.00 jioni na timu zote zimetamba kufanya vyema.
Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary alisema kuwa kalba ya kwenda Wazo, wachezaji wote watafanya mazoezi leo Jumamosi Asubuhi kwenye uwanja wa Kijitonyama (Bora) kuanzia saa 1.30 asubuhi.
Alisema kuwa mara baada ya mazoezi hayo, wachezaji watatawanyika kwenda kwenye majukumu yao na baadaye kukutana tena saa 9.00 alasiri tayari kwa safari.
“Ni mechi ngumu sana, kwani wapinzani wetu wamejiandaa vyema, sisi pia tumejiandaa vizuri na lengo letu ni kupata ushindi,” alisema Majuto.
Mkuu wa Magereza wa Wazo Hill, SP Ipyana Thompson Mwakyusa alisema kuwa wameamua kucheza na Taswa SC ili kudumisha ushirikiano wao na waandishi wa habari.
Mwakyusa alisema kuwa mbali ya mechi ya Taswa SC, pia kutakuwa na mechi nyingine za timu za maveterani za Bocco National Veterans, Bunju Veterans na nyinginezo nyingi.
Alisema kuwa pia kutakuwepo na michezo mingine kama bao, drafti kwa lengo la kupamba siku hiyo wataonyesha eneo la kupumzikia (garden) na bwalo.
“Tunaomba mashabiki wa mpira wa miguu na michezo mingine kufika kwa wingi na kushuhudia mechi kali baina ya waandishi wa habari na askati magereza,” alisema Mwakyusa.