Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Beda Chamatata akifungua kikao cha majumuisho ya NGOs Mapema leo Mkoani Shinyanga.
Baadhi ya viongozi wa NGOs Mkoani Shinyanga wakifutilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa kwao kuhusu mabadiliko ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2019.
Mwanasheria kutpoka Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali Bwana Shewedi Faki akitoa mada kuhusu mabadiliko ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2019.
Baadhi ya viongozi wa NGOs Mkoani Shinyanga wakifutilia kwa makini mada zilizokuwa zinawasilishwa kwao kuhusu mabadiliko ya Sheria ya NGOs ya Mwaka 2019.
…………………………………………………………………………………..
NA MWANDISHI WETU- SHINYANGA
Ofisi ya Msajili wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali imebaini mapungufu mbalimbali katika baadhi ya NGOs Mkoani Shinyanga ikiwemo baadhi ya Mashirika hayo kuwa na usajili lakini hayafanyi kazi kabisa kinyume na matarajio ya Ofisi ya Msajili wa Mashirika hayo.
Akiongea wakati Kikao cha Majumuisho na Mashirika hayo Bi. Jaina Said kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Nchini amesema kuwa baadhi ya mashirika Mkoani Shinyanga hayafanyi kazi kwa kisingizio cha kukosa ufadhili akionya kuwa hayo na mapungufu ya kisheria kwani hakuna Shirika linalosajiliwa na Serikali kwa lengo la kupatiwa ufadhili.
‘’Unaposajili Shirika hakuna mahali Sheria inatamka kuwa utakuwa na ufadhili ila unapokamilisha usajili unatakiwa kuanza kazi kwa bajeti ndogo unayokuwa nayo kwa kuwa Mashirika yanasajiliwa kwa lengo la kutoa huduma kwa jamii na mfadhili hawezi kukuona ukiwa nyumbani kwako.’’ Alisema Bi. Jaina Said Ofisa kutoka Ofisi ya Msajili wa NGOs Nchini.
Aidha Bi. Jaina ameongeza kuwa mapungufu mengine ambayo ofisi yake iliyabaini ni Mashirika hayo kushindwa kuwasilisha taarifa za mwaka akiutaja mwaka wa NGOs kuwa January- Desemba kama Fomu No. 14 iliyopo katika Tovuti ya Msajili inavyotaka Mashirika yote binafsi kuwasilisha taarifa za robo mwaka lakini pia fomu ya NGO namba 10 inayotaka kuwasilisha taarifa ya mwaka pamoja na viambatanisho vinavyoelekezwa na fomu hiyo.
Aidha Ofisa huyo kutoka Ofisi ya Msajili aliongeza kuwa Mashirika Mengi yamekuwa yakifanya mabadiliko mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya Bodi na hata eneo la ofisi bila kutoa taarifa kwa Msajili wa Mashirika kwa kuwa Shirika linaposajiliwa linakuwa na Wasifu wa Viongozi, Mtaa na Bodi hivyo unabodalisha mambo haya ni lazima kutoa taarifa ofisi ya Msajili ili Mabadiliko hayo yaendana na taarifa zako zilizoko katika Ofisi ya Msajili.
Naye Kaimu Afisa Tawala Mkoa wa Shinyanga Bw. Beda Chamatata wakati wa hotuba ya ufunguzi wa Kikao cha Majumuisho hayo ameyataka mashirika Mkoani Shinyanga kuhakikisha yanafanya kazi kwa ukaribu na Serikali Mkoani humo ili kujenga uelewa wa pamoja kuhusu sughuli za Mashirika hayo Mkoani Shinyanga.
Aidha Bw. Chamatata ameyetaka Mashirika hayo kuunda chombo cha pamoja kitakacho yawezesha Mashirika kutambuana pamoja nakujua maeneo ya kufanyia kazi kwa lengo la kuondoa kurudia kazi zilezile japo utekelezaji ni wa Mashirika tofauti.
Kaimu Meneja wa TRA Mkoani Shinyanga akiongea kuhusu maeneo ya NGOs yanayosamehewa kodi aliwambia wajumbe wa kikao hicho kuwa jambo kubwa wanalopaswa kulikumbuka ni kwamba kodi ya mapato katika mishahara ya viongozi na watumishi wao ni la lazima kulipa mapato kama ilivyo kwa watumishi wengine katika maeneo yao ya kazi.
Ofisi ya Msajili wa NGOs Nchini imekuwa Mkoani Shinyanga kuangalia namna Mashirika yanavyofanya kazi lakini pia kujionea ni namna gani Mshirika hayo yanafanyakazi kulingana mabadiliko ya sheria namba 24 ya mwaka 2019.