Waziri wa Maji Profesa Makame Mbalawa akimtwisha ndoo ya maji mwanakijiji mmoja wa Kata ya Nguzogole Manispaa ya Shinyanga alipofika hapo kujionea miradi ya maji inayoendelea Kijijini hapo.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbalawa akionawa mikono katika Mradi wa maji wa kata ya Galamba nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga mradi unaosimamiwa na RUWASA alipofika hapo kujionea miradi ya maji inayoendelea Kijijini hapo.
Waziri wa Maji Profesa Makame Mbalawa akifungua maji ya Mradi wa maji wa kata ya Galamba nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga mradi unaosimamiwa na RUWASA alipofika hapo kujionea miradi ya maji inayoendelea Kijijini hapo.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi Jasinta Mboneko aliyeambatana na Waziri wa Maji Profesa Makame Mbalawa kukagua miradi ya maji ya Manispaa ya Shinyanga akisalimiana na mmoja wa Wanakijiji wa Kata ya Galamba nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga ambaye anaonekana kufurahia kukamilika kwa mradi wa maji kijijini ghapo.
………………………………………………………………………….
Na Mwandishi wetu Shinyanga
Waziri wa Maji Prof. Makame Mbalawa amezitaka Mamlaka za Maji Nchini kuacha kutumia wakandarasi katika miladi ya maji kwani mpaka sasa uzoefu unaonesha miradi yote ya maji Nchini ambayo imekuwa ikitumia wakandalasi imeshindwa kukamilika au haikamiliki kwa wakati na badala yake waendelee kutumia utaratibu wa false account.
Prof. Malawa amesema hayo leo wakati wa ziara yake Mkoani Shinyanga kutembelea miradi ya maji iliyokamilika na inayoendelea ambayo kimsingi imetumia utaratibu wa false account kutekeleza miradi ya maji mkoani Shinyanga.
Profesa Mbalawa utaratibu wa matumizi ya false account tayari umeokoa fedha nyingi za serikali kwani unakuta makadalio ya gharama za mradi yanayowekwa kitaalam na wataalam wa uahandisi wa maji lakini ukitumia utaratibu wa false account unakuta gharama inapungua karibu nusu ya makadilio ya awali.
Akiongea wakati alipotembelea mradi mpya wa maji wa Mawaza- Nyegezi ambao awali ulikadiliwa kuwa kiasi cha fedha za kitanzania bilioni mbili lakini baada ya kutekelezwa kwa utaratibu wa false account mradi huo sasa uko katika hatua ya mwisho na tayari umetumia kiasi cha shilingi bil.1.1 na kuokoa kiasi kikubwa cha fedha.
Aidha Prof. Mbalawa ameitaka Wizara ya Maji kufikilia kutumia wakandalasi pale tu ambapo hawana uwezo wa kutekeleza kwa kuwa tayari Serikali imetekeleza mingi ikiwemo kutengeneza visima vya maji ambavyo sasa vimesaidia kupunguza kero za maji hapa Nchni.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Bi. Jasinta Mboneko amemwomba Prof. Mbalawa kuongeza fedha ya miradi ya maji katika Wilaya Shinyanga ili wananchi ambao wako nje ya miradi ya maji nao waweze kunufaika na kuwapo kwa miundombinu ya maji jilani ya makazi yao suala ambalo Waziri huyo amehaidi kulitekeleza.
Wakati huo Mkazi wa Kata ya Galamba iliyoko nje kidogo ya Manispaa ya Shinyanga Bw. Gabriel Nkwabi ambaye pia ni mnafaika wa mradi wa maji ameishukuru serikali kupeleka maji katika Kijjiji chao kwani imeondoa kero ya kinamama ya kufuata maji mbali na kuomba serikali kuongeza juhudi ili watu wengi wa visima jilani viweze kunufaika na huduma hiyo.
Naye Bi. Janeti John wa Kata ya Uzogole amesema kabla ya mradi wa maji kufika Kijijini hapo wanawake walikuwa wakitukanwa na kupigwa kutokana na kuchelewa katika kutafuta maji katika kijiji jilani cha Mwalugoe lakini sasa umradi umekuwa mkombozi na amani imerudi katika familia.
Waziri Makame Mbalawa anaendelea na ziara yake Wilayani Kahama baada ya kuwa amekamilisha ziara yake katika Manispaa ya Shinyanga ili kukamilisha ziara yake siku ya Siku Mbili inayoenmdelea Mkoani Shinyanga.