Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akiingia kwenye madarasa ya shule ya Msingi Mlali kujionea uchakavu wa majengo na Ukosefu wa madawati unaopelekea watoto kukaa chini kabla ya kutoa Msaada wa Mifuko 100 ya Sarungi.Prof. Chibunda akitembelea moja kati ya madarasa ya shule hiyo na kuongea na wanafunzi.
Mkuu wa shule ya Msingi Mlali Mwalimu Omary Kibukila akizungumza juu ya changamoto ya Madarasa, matundu ya choo pamoja na Ukosefu wa Madawati wakati wa hafla fupi ya kupokea mifuko 100 ya Saruji kutoka SUA. Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda akizungumza na viongozi wa shule, Kijiji na Wazazi kabla ya kukabidhi mifuko 100 ya Safufi kwaajili ya Ujenzi wa madarasa kutokana na watoto wengi kukosa madarasa na kusomea nje.Prof. Raphael Chibunda akikabidhi Mifuko 100 ya Saruji kwa uongozi wa shule na Kijiji Kama mchango wa SUA wa awali kwenye Ujenzi wa madarasa ya shule hiyo ya Msingi Mlali ambayo wanafunzi wansomea chini ya miti. Prof. Raphael Chibunda akikabidhi Mashine moja ya kuvuta maji ya kumwagilia kwa kikundi ya Tukalegoya katika kata hiyo ya Mlali ambacho kipo chini ya Mradi wa RIPAT SUA maradi wa ushirikino kati ya SUA na Shirika la RECODA ambapo kikundi hicho kukuomba Mashine hiyo kusaidia umwagiliaji wa shamba Darasa lao.Mkuu wa shule ya Msingi Mlali Mwalimu Omary Kibukila akizungumza juu ya changamoto ya Madarasa, matundu ya choo pamoja na Ukosefu wa Madawati wakati wa hafla fupi ya kupokea mifuko 100 ya Saruji kutoka SUA. Afisa Mtendaji wa kijiji hicho na Muwakilishi wa Afisa elimu bwana Mwl Ally Mbaraka akitoa neno la shukrani baada ya kupokea Safuji hiyo.Mwenyekiti wa a kikundi cha Shamba darasa cha Tukalegoya akipokea hati ya makabidhiano ya Mashine ya umwagiliaji kutoka kwa makamu mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chinunda Afisa mtendaji wa Kijiji hicho aliyemuwakilisha Afisa Elimu akimuonyesha kitu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda wakati alipotembelea Majengo ya shule hiyo ya Msingi Mlali.
*************************************
Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kimekabidhi mifuko miamoja ya saruji yenye thamani ya shilingi milioni moja na nusu kwa ajiri ya kuendeleza ujenzi wa vyumba 9 vya madarasa katika shule ya msingi mlali iliyopo wilayani mvomero mkoani Morogoro ambayo kwa muda mrefu imekuwa ikabiliwa na changamoto ya upungufu wa madarasa na hivyo kupelekea wanafunzi katika shule hiyo kusomea chini ya miti.
Akikabidhi mifuko hiyo kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo kwa niaba ya kamati ya ujenzi, Naibu Makamu wa mkuu wa Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amesema Chuo kimeguswa na hali iliyopo shuleni hapo mara baada ya kuona wanafunzi wanasomea chini ya mti.
‘’Chuo Kikuu atuwezi kupata wanafunzi kama hawa wanafuzi hawajapita shule ya msingi utakuwa ni muujiza kwaiyo tukadhani ilo siotatizo la wananchi wa mlali na sisi ni tatizo la kwetu,na tulichukua ni tatizo la kwetu kwanza kwa kutambua kazi kubwa inayoendelea kufanywa na Serikali ya awamu ya tano chini ya Raisi wetu mpendwa John Pombe magufuli ‘’Alisema Prof Chibunda.
Prof. Chidunda ameongeza kuwa Serikali imekuwa ikifanya jitihada za dhati ili kuboresha majengo ya Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo lengo likiwa ni kuweka mazingira bora kwa Mwanafunzi kuweza kujifunzia na Mwalimu kufundishia.
Aidha ameitaka kamati ya ujezi shule ya Msingi Mlali kuakikisha inasimamia vyema matumizi ya Saruji hiyo ili iweze kutumika kama ilivyo pangwa na kuhakikisha Madarasa hayo yanakamilika kwa wakati ili wanafuzi wapate mahala pa kujifunzia.
Makamu huyo wa mkuu wa chuo kikuu cha Sokoine cha Kilimo SUA Prof. Raphael Chibunda amewaahidi viongozi wa shule hiyo kuendelea kushirikiana nao katika kuhakikisha miundo mbinu ya shule hiyo inakamilika na kwamba waliochotoa leo ni mwanzo na pindi wapatapo nafasi nyingine wataendelea kuisaidia shule hiyo.
Akizungumza mara baada ya kupokea msaada huo Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo ya msingi Mlali Mwl. Omary Kibukila amekishukuru Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kwa kutoa msaada huo na kuahidi Saruji hiyo kutumika kama inavyo takiwa.
Pia Mwl.Kibukila amesema Shule hiyo inakabiliwa na upungufu wa madarasa 35 kati 43 yanayoitajika huku mpaka sasa madarasa yanayotukia yakiwa ni nane tu, huku upungufu wa vyoo katika shule hiyo ukiwa ni matundu 35 kati ya 41 vinavyitajika kwa wavulana na upande wa kike upungufu ukiwa ni 51 kati ya 60.
Kwa upande wake Afisa Elimu Kata ya Mlali Mwl. Ally Mbaraka amesema baada ya kuona changamoto hiyo ya upungufu wa madarasa katika shule hiyo Serikali ya Kijiji pamoja na kata ilijipanga na kuanza ujenzi wa vyumba vya madarsa vitatu ambavyo vinatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi wa tisa mwaka huu.
Pia ameongeza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero imeisha weka mpango wa kujenga vyumba vya Madarasa tisa ifikapo mwezi wa kumi na moja huku Serikali kuu ikiwa tayali imeleta kiasi cha shilingi milioni 40 ambazo zitatumia kukamilisha ujezi wa madara pamoja na kuweka Madawati.
Shule ya msingi Mlali inajumla ya wanafunzi 2,227elfu ambao wamegawanywa katika makundi matatu.
Katika hatua nyingine Chuo Kikuu Cha Sokoine Cha Kilimo SUA kimekabidhi mashine ya kuvuta maji kwa Kikundi cha Wakulima cha TUKALEGOYA kilichopo katika Kijiji cha mlali kata ya Mlali wilayani mvomero ambacho kinafanya kazi chini ya usimamizi wa Mradi wa RIPAT SUA ambao unatekelezwa kwa ushirikiano kati ya SUA na Shirika la RECODA lenye makao makuu yake Jijini Arusha.
Makabidhiano yam ashine hiyo ya maji yamekuja baada ya maombi yaliyotolewa na kikundi hicho siku ya Mkulima shambani ambapo walisema wanapata tabu sana kumwagilia shamba darasa lao wakati wa kiangazi kutokana na kufuata maji kutoka mtoni hivyo upatikanaji wa mashine hiyo utarahisha umwagiliaji na kuwezesha shamba darasa hilo kufanya kazi mwaka mzima na wakulima kujifunza