……………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu.
Aliekuwa Mbunge Wa Jimbo la Nkenge Balozi Dkt. Diodorus Kamala, ameahidi kuwa ataendelea kutoa msaada wa kuwasomesha vijana elfu moja kupata mafunzo ya elimu ya ufundi stadi yatakayowawezesha kujiajiri.
Akizungumza na waandishi wa habari ,Balozi Kamala amesema kuwa atahakikisha anatimiza malengo hayo, kwa hali yoyote akiwa mbunge au akiwa mtu wa kawaida.
Balozi Kamala katika Uchaguzi wa kura za maoni alishindwa kutetea kiti chake cha Ubunge katika jimbo la Nkenge kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (Ccm).
Hatua hiyo imewapa wasiwasi vijana ambao wengi wao wapo katika chuo cha ufundi stadi cha Maendeleo ya wananchi Gera, kwa msaada wa Balozi Kamala.
Hata hivyo Katika kufanikisha adhma yake ya kuwasaidia vijana wa jimbo hilo, Balozi Kamala, amefungua ofisi binafsi ambayo itakayohusika na maswala ya kusimamia miradi aliyoianzisha kwa lengo la kuwaletea maendeleo wananchi, ikiwemo huo wa kuwasomesha vijana elfu moja.
Kamala amesema mpaka sasa Mafunzo hayo ambayo yanatolewa kwa muda wa miezi mitatu, mpaka sasa jumla ya vijana 140 wananufaika nayo ambapo ifikapo mwezi Oktoba mwaka huu vijana wengine 100 wataanza mafunzo hayo.
Mafunzo wanayopatiwa katika chuo hucho ni pamoja na ufugaji nyuki, kilimo Cha mbogamboga, ushonaji, umeme wa majumbani, computer na ujasiriamali.